Chai Bora Yaasa Watanzania Kuunga Mkono Bidhaa Za Ndani - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, July 7, 2020

Chai Bora Yaasa Watanzania Kuunga Mkono Bidhaa Za Ndani

Meneja masoko chai Bora Awatif Bushiri akizungunza na wanahabari hii leo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Chai Bora ambayo ni watengenezaji na wafungashaji maarufu wa chai nchini Tanzania, wamepongeza juhudi za serikali katika kusaidia viwanda vya ndani. Hayo yamesemwa na Awatif Bushiri, Meneja Masoko wa Chai Bora wakati wa Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam.

"Kama inavyojidhihirisha kwenye kauli mbiu ya mwaka huu isimayo Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu, serikali imeweka mazingira mazuri kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kipato cha kati kupitia Viwanda. Tunashukuru kwa juhudi za serikali katika kukuza viwanda vya ndani kupitia majukwaa mbali mbali. Kama kampuni ambayo pia inalenga kuuza katika soko la nje katika nchi za Kenya, Afrika Kusini, UAE, Rwanda na Ghana, maonyesho haya ni moja ya njia tunazotumia katika kukuza usambazaji wa bidhaa zetu." alisema Awatif.

Kilimo ni sekta muhimu wakati nchi inapoingia kwenye uchumi wa kipato cha kati kupitia viwanda. Takribani asilimia 75 ya nguvu kazi huishi katika maeneo ya vijijini na wengi wao wanajishughulisha na shughuli za kilimo ambacho huchangia karibia asilimia 50 ya pato la taifa.

Chai Bora inajivunia kuwa na bidhaa zinazotumika na Watanzania wengi, na zaidi inavijunia nafasi za ajira zinazotengenezwa, kuanzia ajira viwandani mpaka ajira mashambani ambapo malighafi huzalishwa.

Akiendelea kuelezea, Awatif alisema, "Licha ya janga la hivi karibuni la virusi vya corona, tunafurahi kuwa serikali inaendelea kukuza viwanda vya ndani kupitia majukwaa kama Sabasaba huku ikiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona."

Hali ya sasa ya kilimo inatoa fursa kubwa ya kusaidia ukuaji wa viwanda na kuzalisha kipato kwa Mtanzania mmoja mmoja. "Hadi sasa kilimo kinachangia sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya nchi, na bado kuna nafasi ya kukua zaidi. Tunawasihi wazalishaji wengine wa ndani kutumia Maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara kama fursa ya kutafuta masoko nje ya nchi, na tunawasihi Watanzania kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini." alihitimisha Awatif.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages