MKUU WA WILAYA YA ARUMERU JERRY MURO AISHAURI NDAGO TV KUTANGAZA UTALII ULIOPO KATIKA MKOA WA ARUSHA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, July 26, 2020

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU JERRY MURO AISHAURI NDAGO TV KUTANGAZA UTALII ULIOPO KATIKA MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya Habari, Mara baada ya kufanya uzinduzi wa kituo kipya cha televisheni NdagoTv, kilichoanzishwa Mkoani Arusha kwa lengo la kusaidia jamii katika kutatua mambo mbalimbali.kulia kwake ni Phidesia Mwakitalima Mkurugenzi msimamizi wa NdagoTv, Kulia kushoto kwake ni Faustine Mwandago Mkurugenzi Mtendaji wa NdagoTv
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akikata utepe, kuashiria uzinduzi wa kituo kipya cha televisheni kijulikanacho kama NdagoTv. (Picha zote na Jane Edward)

Na Jane Edward, Arusha

Mkuu wa  Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amekitaka kituo Cha kurusha matanganzo Ndago Tv kilichopo jijini Arusha kutangaza utalii ili kuendelea kutanganza kituo hicho pamoja na kukuza utalii uliopo mkoani hapo.

Amezungumza hayo wakati akizindua kituo hicho cha matangazo cha kwanza mkoani hapo pamoja na kutoa  tunzo kwa washiriki walioshiriki katika  kutafuta watangazaji bora wa television  hiyo ambapo amesema  kuna haja kubwa yakufanya vipindi vya utalii  kwa asilimia 70 kwani kituo hicho kipo ndani ya mkoa wa Arusha kulingana na jambo kubwa katika mkoa huo ni utalii.

Jerry amesema kuwa kwa utalii ndani ya mkoa huu ndio jambo kubwa hivyo kituo hicho kinaweza kikatumia fursa hiyo ya kujitangaza hata kwawadau wa utalii na kuwarahisisha wakazi wa arusha kutalii kwa kuangalia vipindi hivyo.

Hata hivyo Muro amesema kufunguliwa kwa kituo hicho kitasaidia vijana wengi wenye taaluma ya habari kuweza kupata ajira na kuendelea kukuza wigo ya tasnia ya habari pamoja na kuendelea kukuza uchumi wa nchi kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano juu ya kuboresha ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msimamizi wa Ndago TV Phide  Mwakitalima  amesema kuwa wanamshukuru mkuu huyo wa wilaya hiyo kwa ushauri huo kwani hadi Sasa wanampango wakuanzisha vipindi vya utalii na tayari wameshawasiliana na TANAPA na muda mfupi wataanza kurusha vipindi hivyo vya utalii  ili kuendelea kutanganza utalii pamoja na kukuza kituo hicho Cha TV katika makampuni mengi.

Mwakitalima amesema lengo la kufunguliwa kwa kituo  hicho cha televisheni ni kuhakikisha vijana wa mkoa huo kuingia katika ajira ya habari na kupinguza vijana waliopo mtaani kwani Hadi Sasa wametoa ajira kwa vijana 18 na ambao hawajaingia katika ajira wapo 10 huku lengo lao la kuajiri katika kituo hicho Ni waajiriwa kufikia 50.

Hata hivyo kituo hicho kilianzisha mashindano ya kuwatafuta watangazaji Bora katika mkoa ili kuweza kuwapatia ajira hivyo katika mchujo wa wamewapa a washindi 5 na Kati ya hao  wawili wanaenda moja kwa moja kwenye ajira na wengine watakuwa sehemu ya shughuli za televisheni.

Amefafanua  kuwa kuanzia  August 1 hadi Agosti 8 wataanza kuzungumza na wajasiriamali mubashara  ili kuendelea kuitagaza television hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Ndago TV Fautine Mwandago amesema anaishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana naye hadi kufikia kuwekeza kituo hicho cha matangazo  kwani ilikuwa ilikuwa ndoto yake ,

"Mwaka 2015 niliweza kushauriwa na kusaidiwa na waandishi na ilipofika mwaka 2016 nilianza mchakato wa kufungua kwa kutafuta kibali TCRA  na 2019 nilipewa kibali cha kupiga muziki tu ndipo ilipofika Februari 2020 nikapewa kibali rasmi cha kuanza kurusha vipindi na matangazo  tukiwa tumeanza na vipindi saba wakati sasa tuna vipindi 19," amesema.

Hata hivyo ametoa ombi kwa kampuni mbalimbali kujitokeza kuja kurushiwa matangazo yao ili kufanikisha kituo hiko kuendelea kusonga mbele kwa kukizi mahitaji ya katika kuendesha tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages