Saturday, July 11, 2020

Morrison aomba kupangwa kikosi cha kwanza ili kuimaliza Simba
BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga, amesema kuwa anamuomba Kocha Mkuu, Luc Eymael ampange kwenye mchezo huo ili afanya kazi yake mbele ya Simba.
Yanga itamenyana na Simba, kesho Julai 12 Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Morrison alikuwa na mvutano wa kimkataba na masuala ya nidhamu na baadhi ya viongozi wa klabu yake ila kwa sasa amesharejea kambini na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi.
Morrison amesema: “Nikipata nafasi ya kucheza nitaendelea kulinda heshima yangu na ya klabu, muhimu naomba Mungu niwe na afya njema kisha kocha anipe nafasi ya kucheza.
“Ninachohitaji ni sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono tangu nimefika hapa Tanzania, kama timu tunataka kuendelea pale tulipoishia.
“Tunahitaji matokeo mazuri ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao, muhimu naomba kocha anipe nafasi kama nitakuwa fiti kiafya kisha mashabiki watuunge mkono katika mchezo huo muhimu."
Tags
# MICHEZO
Share This
About kilole mzee
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
TANTRADE YAISHUKURU BENKI YA NBC KWA KUWADHAMINI WAJASIRIAMALI
Older Article
ALICHOKISEMA DKT HUSSEIN MWINYI BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
Hassani MakeroMar 08, 2025WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA KUSHIRIKI MBIO ZA YAS KILI INTANATION HALF MARATHON
kilole mzeeFeb 15, 2025KOCHA WA YANGA APEWA MKONO WA KWAHERI
Hassani MakeroFeb 04, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment