Thursday, July 2, 2020

MWALIMU akamatwa kwa WIZI wa MILIONI 34!
Na Esther Macha, Mbeya
MWALIMU wa Shule ya Msingi Mwakareli, Joseph Shila (29) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za wizi fedha shilingi milioni 34 ambazo ni mali ya Mwalimu Mstaafu Gideon Mwalujobo (60) mkazi wa Mwakareli mkoani humo.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa alikamatwa June 30 mwaka huu saa moja usiku katika Kata ya Mwakareli, Tarafa ya Busokelo, wilayani Rungwe.
Amesema kuwa baada ya polisi kupata taarifa toka kwa msiri na kwamba mtuhumiwa alifanikiwa kuiba fedha hizo za mwalimu mwenzie kupitia akaunti kwa kutumia NMB Mobile katika Tawi la Mbalizi Road baada ya kupata namba ya siri ya Mwakujobo.
Aidha Matei ameongeza kuwa Mwakujobo alikuwa ni walimu wa shule Moja na marafiki wa siku nyingi na mtuhumiwa.
Amesema pia mtuhumiwa pia anajihusisha na uwakala wa kusajili laini za simu kwa kutumia mfumo wa kisasa wa alama za vidole ambapo aliweza kutengeneza laini ya simu kwa jina la Mhanga na kutokana na kuaminiana na mhanga pia alikuwa ana mpa kadi yake ya benki kwa ajili ya kumtolea fedha..
Katika upekuzi uliofanywa nyumbani kwa mtuhumiwa amekutwa na fedha taslimu Tshs. Milioni 20,780,000/=, Kadi ya Benki NMB, Simu tatu aina ya Tecno na laini mbili za simu.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kadi zao za benki ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatunza namba ya siri ili kujiepusha na matukio ya wizi.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
DTB BANK FC QUALIFIES FOR "SUPER SIX LEAGUE" THAT WILL BE STAGED IN LINDI FROM 4 JULY, 2020
Older Article
MATOKEO YA TUNZO YA TANO YA FILAMU INAYOTOLEWA NA MFUKO WA EMERSON'S ZANZIBAR FOUNDATION KUTANGAZWA JULAI 4
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment