Wednesday, July 8, 2020

WAZIRI JAFO ATAKA DAMPO LA KISASA JIJINI TANGA LILINDWE
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo Jijini Tanga.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo kushoto akizindua Jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga leo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
NA: MWANDISHI WETU, TANGA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo ametaka dampo la kisasa la Mpirani Jijini Tanga lilindwe kwa sababu ni uchumi na limetumia kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wake mpaka lilipokamilika huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kwenda na viroba kuchukua kokoto.
Amesema kwani kokote hizo zimemwagwa kwenye dampo hilo kwa ajili ya kulinda dampo hilo ambalo litakuwa la kisasa kwa Jiji hilo tokea lilipoanzishwa huku akieleza ujenzi huo umetokana na mapenzi mwema ya serikali ya awamu ya tano Dkt John Magufuli kuwadumia watanzania.
Jafo aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake Jijini Tanga ambapo alitembelea mradi mbalimbali na kufanya uzinduzi ambayo ni ujenzi wa dampo la kisasa mpirani, ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Jiji hilo,Ujenzi wa mradi wa mkakati wa Jengo la kitega uchumi stendi ya mabasi.
Baada ya kutembelea dampo hilo alionekana kuridhishwa na ujenzi wake huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na watendaji wake ikiwemo wasimamizi wa mradi huo kutoka Tarura Makao Makuu.
Sambamba na maeneo hayo lakini pia Waziri huyo alitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Kange stendi kuu ya mabasi ambapo kote alipopita alionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema katika maeneo mengine ya dampo wakati unapokwenda kutembelea unaona hofu ya kufika lakini kwenye dampo hilo tokea nimefika hapo sikikii harufu yoyote hivyo mkurugenzi na watendaji wake mmefanya kazi kubwa sana.
Waziri huyo alisema mradi huo umepata umepata mafanikio makubwa kwani Tanga ya mwaka 2015 sio ya mwaka 2020 hivyo dada zangu walikuwa na viatu vya mchuchumio na nywele wanaweza kutengeneza vizuri lakini wanashindwa kutembea lakini kwa sasa wanaweza kutembela bila kuwepo na hofu.
“Pongezi kwa Jiji la Tanga ujenzi wa hospitali ya wilaya eneo la Masiwani mmepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya leo nimepata taarifa huduma zinatolewa na Rais ametoa fedha nyengine za ujenzi wa vituo vyengine hapa Tanga maana yake wananchi waliokuwa wanatembela umbali mrefu sasa watapata huduma karibu tena vituo vilivyoboreshwea kwa kisasa”Alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo alisema kwamba watumishi wa halmashauri msingesimama pamoja kwa ajili ya miundombinu hiyo ambayo imejengwa kwa gharama ya milioni 400 mpaka milioni 500 wakati vituo hivyo kipindi cha nyuma vilikuwa vinajengwa kwa wastani wa bilioni 2 wakaelekeza vituo hivyo vijengwa kupitia fedha ya ndani (Force Acount).
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
WENYE VIWANDA WAPEWA ELIMU YA MATUMIZI BORA YA NISHATI YA UMEME
Older Article
KATIBU MKUU WA CCM, DK. BASHIRU ALLY APOKEA GARI MAALUM LA KAMPENI, JIJINI DODOMA
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment