Wamiliki wa Viwanda Wilaya za Dodoma na Bahi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya ukarabati wa mara kwa mara na kubadili vifaa vilivyo tumika kwa muda mrefu ili kuepuka gharama zisizo za lazima na matumizi makubwa ya nishati ya umeme.
Wito huo umetolewa na Mhandisi mtafiti wa Tanesco, Aurea Bigirwamungu wakati wa kutoa elimu juu ya matumizi bora ya Nishati ya Umeme katika wilaya za Dodoma na Bahi.
Naye Ofisa Tawala wa Kampuni ya Nyanza Road Workers, Bakari Mugini ameishukuru Tanesco kwa mafunzo yaliyofanya kujua namna ya matumizi sahihi ya nishati hiyo.
Mugini ameeleza kuwa katika mafunzo hayo wamepata elimu juu ya usalama wa miundombinu iliyopo katika viwanda ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment