Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wilayani humo wameandaa kambi kwa vijana 100 ili wapate nafasi ya kukumbushwa miiko na maadili ya chama hicho.
Mwegelo amesema lengo la kambi hiyo ni kufanikisha ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kambi hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kisarawe, Asha Msonzo, amesema vijana hao watakaa kambi kwa siku tano maalumu kwa ajili ya kupeana mikakati mbalimbali ya CCM ili kufanikisha ushindi wa CCM.
No comments:
Post a Comment