Mnamo mwaka 1934! Kikundi cha wafungwa hatari zaidi katika Serikali ya Marekani waliletwa kwenye Kisiwa cha Alcatraz waliohukumiwa kufungwa wakiungana na wafungwa kadhaa wa kijeshi waliokuwepo kwenye gereza hilo la jeshi la Marekani.
Alcatraz ilikuwa bandari ya bahari isiyokuwa na makazi wakati ilipogunduliwa na Spanish Lieutenant Juan Manuel de Ayala mnamo 1775 umbali wa Mile 1.25 (2.01 km) kutoka katika Pwani ya San Francisco, California, katika nchi ya Marekani.
Juan alikipa kisiwa hiki jina la “Isla de los Alcatraces” au Kisiwa cha Wapeliki.
Kisiwa hichi cha Alcatraz kiliuzwa kwa Marekani mnamo 1849.
Kuanzia mnamo 1859, jeshi la Marekani lilikitumia kisiwa hicho kama gereza hivyo kutoka mwaka 1868 gereza la Alcatraz lilitumiwa kuweka wahalifu wa kijeshi wa jeshi la Marekani.
Mnamo mwaka 1907, Alcatraz iteuliwa kuwa Tawi la Pasifiki la Gereza la Kijeshi la Marekani hadi mwaka 1934 lilipotambulishwa kuwa ni moja ya gereza la shirikisho la usalama Marekani “High-security federal penitentiary”.
Ingawa watu kadhaa walijaribu kutoroka kutoka katika gereza hilo, hakuna mfungwa aliyejulikana kufanikiwa kutoroka kwenye kisiwa hicho kilichojulikana kama "The Rock"
Mnamo 1963, Wakili Mkuu wa Marekani Robert F. Kennedy aliamuru Alcatraz kufungwa hivyo Kufikia mwaka 1972, Alcatraz ilikuwa wazi kwa umma kama sehemu ya Makumbusho ya Kitaifa ya Golden Gate.
Alcatraz Cellhouse
No comments:
Post a Comment