MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akichukua fomu ya kuomba kuwania nafasi hiyo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanga Daudi Mayeji.
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwaonyesha fomu za kuwania Ubunge Jimbo la Tanga mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga.
Umati Mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kumsindikiza Waziri Ummy wakati alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga eneo la Masiwani Jijini Tanga.
Waziri Ummy kushoto akiwa na Wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga CCM wakati alipokwenda ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa na chama chake.
KATIBU wa CCM wilaya ya Tanga Salum Kidima akizungumza
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na wananchi na wana CCM wakati alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amelitikisa Jiji la Tanga wakati alipokwenda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo huku akiwa amesindikizwa na umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto msafara wake ambao ulikuwa ukisindikizwa na magari, pikipiki huku wananchi wengine wakiwa pembezoni mwa barabara wakimshangilia na kumpungia mikono.
Msafara huo ulizunguka maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo na baadae kufika kwenye ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kuwania kiti hicho.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Ummy alisema kwamba anawashukuru halmashauri kuu ya CCM kwa kumwamini na kumpitisha kuwania Ubunge Jimbo la Tanga huku akiahaidi kufanya kampeni za kiistarabu shuka kwa shuka, kitanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu.
Alisema kwa anawashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Tanga ambao walimpitisha kwa kura za kishindo kwa kumpendekeza kuwa mgombea wa Ubunge Tanga mjini.
“Wajumbe wamekuwa ni watu maarufu sana lakini wajumbe wa mkutanbo mkuu wa Tanga mjiniwaoi kwangu mimi wamenitendea haki kwangu mm wamenipa heshima niwashukuru sana wenyeviti wa ccm kutoka matawi yote 153 ya jiji la Tanga, makatibu tawi wote, na makatibu wenezi wote pamoja na wajumbe waliotoka kwenye ngazi ya matawi,’’ alisistiza Ummy Mwalimu.
Nilipata heshima ya kuwa Mbunge viti maalumu miaka 10 na mshahara wa mbunge wa viti maalumu na jimbo ni mshahara mmoja ningekuwa nimeshamaliza mchezo lakini kwasababu ya shauku na mapenzi makubwa kwa wanantanga hulka na hamu yangu ya kuipenda Tanga mjini ninataka kuiona yenye heshima na hadhi yake", amesema.
Aidha Waziri Ummy alituma salamu kwa wapinzani wake kuhakikisha wanajipanga vyema kwani wao watafanya kampeni za maendeleo na kampeni za kistaarabu na heshima, kampeni zinazoakisi hadhi, utu na heshima ya wanatanga kutokana na hulka ya wanatanga kuwa wastaarabu.
No comments:
Post a Comment