Absa Tanzania yahitimisha mafunzo kwa Waandishi wa Habari za Biashara - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, September 10, 2020

Absa Tanzania yahitimisha mafunzo kwa Waandishi wa Habari za Biashara

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania Hellen Siria (kulia) akimkabidhi mfuko wenye zawadi mbalimbali kutoka kwenye Benki hiyo mwandishi aliyeshiriki mafunzo maalum ya 'Absa Data Journalism Master Class' Rachel Chacha (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ya siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania Hellen Siria (wa kwanza kushoto) akiwa amejumuika na waandishi wa habari mbalimbali katika mafunzo maalumu ya 'Absa Data Journalism Master Class' yaliyotolewa kwa njia ya Video na Mkufunzi Peter Verweij kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes kilichopo Afrika Kusini. Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili Septemba 9, na Septemba 10,2020 kwa udhamini wa Benki ya Absa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Benki hiyo Jijini Dar es Salaam.



Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwemo wa mitandao ya kijamii wakiwa kwenye Mafunzo maalum ya siku mbili ya 'Absa Data Journalism Master Class' iliyomalizika Semtemba 10, 2020 Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yametolewa kwa njia ya Video kutoka Afrika Kusini na Mkufunzi Peter Verweij wa Chuo Kikuu cha Rhodes kilichopo Nchini humo.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania Hellen Siria (wa kwanza kushoto) na waandishi wa habari wengine wakiwa Darasani kufuatilia mafunzo hayo kwa njia ya Video.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania Hellen Siria (mwenye miwani) akiwaonesha Jambo baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki Mafunzo maalum ya 'Absa Data Journalism Master Class' yaliyofanyika kwa njia ya Video kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki hiyo Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki Mafunzo ya 'Absa Data Journalism Master Class' wakielekezana Jambo walipokuwa Darasani kushiriki Mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages