DC ILALA AZISHUKIA KAMPUNI FEKI ZA UPIMAJI VIWANJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, September 10, 2020

DC ILALA AZISHUKIA KAMPUNI FEKI ZA UPIMAJI VIWANJA



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Gw'ilabuzu Ludigija akipokelewa na Katibu wa Umoja wa Wanawake Kata ya Buyuni Aziati Juma leo ofisi ya Kata katika ziara endelevu ya mkuu wa Wilaya kutatua kero za Wananchi.

Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ukonga Mponjoli Damsoni akielezea serikali ilivyojipanga kutatua kero ya maji Jimbo la Ukonga (Picha zote na Heri Shaaban).

Na Heri Shaaban, Dar es Salaam
MKUU wa WIlaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija ametoa agizo kwa Afisa Ardhi Manispaa ya Ilala kuzihakiki upya Kampuni za Urasimishaji ardhi zilizopo manispaa ya Ilala na kuzichukulia hatua kampuni feki.
Mkuu wa Wilaya Ludigija alitoa agizo hilo Kata ya Buyuni Jimbo la Ukonga leo  katika ziara yake endelevu Wilayani Ilala ya kutatua kero za Wananchi.
Ludigija alisema Kampuni zote za urasimishaji ardhi zilizochukua tenda ndani ya wilayani Ilala kama  kazi hawajamaliza na mkataba umekwisha warudishe fedha za wananchi na Wizara wawafute hazifai.
"Kuna kampuni za urasimisha zinafanya utapeli nimepitia taarifa moja ya kampuni iliyochukua tenda Kata ya Buyuni toka mwaka 2019 mpaka sasa mkataba umekwisha kazi bado hajamaliza na kuleta kero kwa wananchi wamepeleka michoro Wizarani wamerudishwa naomba warudishe pesa kwa wananchi" alisema Ludigija.
Alisema kampuni hiyo ilipewa mkataba miezi nane wawe wamemaliza kazi waliopewa.
Alitoa agizo kwa Afisa Ardhi Manispaa ya Ilala kuzifanyia uhakiki upya kampuni zote za urasimishaji zilizopewa tenda kuangalia  mikataba yao kama kazi walipewa wamemaliza wasitumie ujanja ujanja na kama wameshindwa kazi hizo zitafanywa na wataalam wa manispaa ya Ilala.
Alisema wananchi wakipata hati zao watakuwa rais kukopesheka na kuchukua mikopo mikubwa .
Kwa upande wake Meneja  DAWASA Mkoa wa Ukonga Mponjoli Damsoni alisema sekta ya maji kuna mradi mkubwa wa maji wa Kisarawe Mkoa wa Pwani mara baada kukamilika mradi huo utasambaza maji katika kata za Majohe,Chanika ,Buyuni ,Pugu na mpaka Kivule  dhumuni kumaliza changamoto ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Jimbo la Ukonga.
Damsoni alisema mradi huo mkubwa wa Serikali  mikakati hiyo mpaka kufika Desemba mwaka huu DAWASA itakuwa imemaliza kazi na  kusambaza maji maeneo mbalimbali ya jimbo la ukonga ulipopita mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages