Kwa mujibu wa shirila la elimu, syanasi na utamaduni Unesco limesema kuwa nusu watoto katika ufunguzi wa mwaka wa shule ndiyo watakaoweza kuingia madarasani kutokana na sintofahamu iliyogubika maeneo mengi ya dunia sasa hivi kutokana na vizuizi vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 na sababu nyinginezo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema muhula mpya wa masomo alianza Agosti hadi Oktoba mwaka huu, theluthi moja ya wanafunzi bilioni 1 nukta 5 wa shule za awali hadi sekondari ndio wamejiandaa kurejea shuleni. UNESCO hata hivyo katika taarifa yake iliyotolewa jijini Paris, Ufaransa, imesema ni nusu yao hao tu ndiyo watakaoweza kuingia madarasani kutokana na sintofahamu iliyogubika maeneo mengi ya dunia sasa hivi kutokana na vizuizi vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 na sababu nyinginezo.
Kwa mujibu wa UNESCO inasema nusu hiyo ambayo ni sawa na watoto milioni 488 wataweza kujifunza kwa mbinu mchanganyiko ikiwemo kujifunzia wakiwa nyumbani au kuingia madarasani, “ingawa idadi kubwa bado inasubiri muongozo wa kile wanachotarajia wakati siku za kufungua shule zimekaribia.” Shirika hilo linasema kuwa hali hii ni tatizo kubwa ikizingatiwa ukosefu wa usawa utokanao na wanafuzi kusomea majumbani, hali itakayoathiri jamii zilizo hatarini zaidi.
Akizungumzia sintofahamu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema “Janga la elimu linasalia kuwa tatizo kubwa, vizazi kadhaa vinakumbwa na tishio la shule kufungwa, hali inayotia hofu kwa mamilioni ya wanafunzi na imedumu kwa miezi kadhaa. Hii ni dharura kwa elimu duniani.” Leo hii, wanafunzi duniani kote wamepoteza wastani wa siku 60 za masomo shuleni tangu vizuizi vya COVID-19 vianze mwezi Februari na Machi mwaka huu.
UNESCO inasema katika mazingira kama hayo suala la utoro shuleni, kupungua kwa ubora wa elimu na madhara yake kiuchumi na kijamii ni bayana.
No comments:
Post a Comment