STAND MPYA MBEZI LUIS KUANZA KUTUMIKA RASMI NOVEMBER 30, MAJARIBIO KUANZA NOVEMBER 25 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, November 9, 2020

STAND MPYA MBEZI LUIS KUANZA KUTUMIKA RASMI NOVEMBER 30, MAJARIBIO KUANZA NOVEMBER 25





Na Mwandishi wetu | Dar es Salaam | Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema Ujenzi wa Stand mpya ya Mabasi ya mikoani ya Mbezi Luis umefikia 90% na itaanza majaribio ya Kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30.

Kutokana na hilo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stand hiyo ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hotel ambapo zoezi la kutuma maombi limeanza leo November 09 Hadi November 25.

Aidha RC Kunenge amesema uwepo wa stand hiyo itaendelea kufungua fursa za maendeleo kwa Wakazi wa Ubungo hivyo amewataka kujiandaa kwa hilo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages