Dkt.Abbasi Atuma Salamu Kwa Watanzania Kuwa Maandalizi Ya Tamasha Yamekamilika - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, December 25, 2020

demo-image

Dkt.Abbasi Atuma Salamu Kwa Watanzania Kuwa Maandalizi Ya Tamasha Yamekamilika

PIX-1-14-2048x1365
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akituma salaam kwa wana Dar es Salaam, Tanzania na Afrika kwa ujumla kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival kuwa limewadia na litafanyika tarehe 26, Desemba 2020 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tamasha hilo.
PIX-2-16-scaled
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID akiwahakikishia mashabiki zake kuwa amejipanga kutoa burudani ya viwango vya hali ya juu hivyo wasanii wengine nao wajipange kwani hili ni tamasha kubwa sana na watanzania wanatarajia show nzuri, jana Desemba 24, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tamasha la Serengeti Music Festival.
PIX-34-scaled
Msanii wa Muziki Mrisho Mpoto akitoa shukrani kwa Serikali kwa kuandaa Tamasha la Serengeti Music Festival huku akieleza orodha ya wasanii watakoshiriki tamasha hilo kuwa kubwa hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Uhuru kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii hao,katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana Desemba 24, 2020 .
PIX-4-9-scaled
Msanii wa Muziki wa Hip Pop Kala Jeremiah akitoa shukrani kwa Serikali kwa kuandaa Tamasha la Serengeti Music Festival kwani limeleta hari mpya kwa wasanii kwa na kuonyesha dhana ya serikali kujali Wasanii na kuthamini mchango wao, jana Desemba 24, 2020, katika mkutano na waandishi wa habari wa kutoa taarifa ya maandalizi ya tamasha hilo, uliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Anitha Jonas – WHUSM | Dar es Salaam | Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ametuma salamu kwa Wana Dar es Salaam, Watanzania wote na Afrika kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival limewadia na litafanyika Desemba 26, 2020 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo jana Desemba 24, 2020 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Serikali kwa lengo la kuanzisha uhusiano wa karibu kwa sekta ya Sanaa na Utalii.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Dkt. Abbasi alisema tamasha hilo litakua ni shukran ya mchango wa wasanii wazamani ambao wamesaidia ukuaji wa tasnia ya Muziki nchini kutoka kuonekana kama jambo la kihuni mpaka kuonekana kuwa chanzo cha kuchangia pato la mmoja mmoja na taifa.

Serikali imesikia kilio cha Wasanii wengi kuhusu Taifa kutokuwepo kwa tuzo zinazoandaliwa hapa nchini hivyo basi mwezi Machi, 2021 tutakuwa na Tuzo. Tutaanda tuzo hizo na Wasanii tunaomba kwa atakayeshindwa basi akubali na asiende kulalamika popote” alisema Dkt. Abbasi.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali alisema baada ya Tamasha hilo, tarehe 27, Desemba 2020 kutakuwa na mwendelezo wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni litakalofanyika Bagamoyo katika chuo cha TaSuBa, na huko kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.

Naye Msanii wa Hip Pop Kala Jeremiah ameishukuru Serikali kwa kuandaa tamasha hilo, huku akisema anaamini kuwa tamasha hilo limeanzishwa katika kipindi cha sherehe za Krismas litaendelea kuwa tamasha kubwa hapa nchini na Afrika.

Halikadhalika kwa upande wa Msanii Khalid Mohamed maarufu kama TID alitoa shukran kwa Serikali nakuwahakikishia watanzania kuwa amejipanga kutoa burudani ya uhakika hivyo mashabiki zake wasikose kufika uwanjani siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *