Rais Magufuli Asali Krismasi Chamwino, Awataka Watanzania Kumshukuru Mungu Kuwaepusha Na Korona - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, December 25, 2020

demo-image

Rais Magufuli Asali Krismasi Chamwino, Awataka Watanzania Kumshukuru Mungu Kuwaepusha Na Korona

27d62144-ded9-42e4-a28a-2304e3ea133d
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika Misa Takatifu ya Krismasi katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo Disemba 25, 2020.
f51398d5-ade5-4489-ac39-4b24cca71f346a80c6a3-2e8d-4ac5-8321-7e8e3bd83c40 9a8b2d49-58ac-46cb-8297-8fedd8c44dd0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitisha kwa waumini kapu la sadaka aliposhiriki katika Misa Takatifu ya Krismasi katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo Disemba 25, 2020.
99012ae0-d1e4-40ed-aab5-3faffad33d24
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini wenzie aliposhiriki katika Misa Takatifu ya Krismasi katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo Disemba 25, 2020.

Katika ibada hiyo Rais Dkt. Magufuli pia amepitisha kapu la sadaka kwa waumini wa kanisa hilo.

Baada ya Misa hiyo iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Paul Mapalala, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza na kuwatakia heri Watanzania wote kwa sikukuu ya Krismasi na amewataka kuendelea kumshukuru Mungu kwa miujiza na upendo mkubwa anaolitendea Taifa la Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli amesema upendo na miujiza ya Mungu kwa Tanzania inajidhihirisha katika kipindi hiki ambapo dunia inapita katika wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Corona (Covid-19) ambapo maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha kila siku, lakini Tanzania imeepushwa na janga hilo na maisha ya Watanzania yanaendelea kama kawaida.

Amewaomba Watanzania wote waendelee kumshukuru na kumuomba Mungu aendelee kulilinda Taifa lao dhidi ya ugonjwa huo, na kuwaombea wananchi wa Mataifa mengine waepushwe na Corona.

Ametoa wito kwa viongozi wa Mataifa mbalimbali duniani kukubali kumuweka Mungu mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona badala ya kutegemea nguvu za binadamu pekee.

Pamoja na kuwatakia heri ya Krismasi, Mhe.Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali ili kuendelea kujenga Taifa lao pamoja na kuhakikisha wanamtanguliza Mungu kwa kila jambo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *