Friday, December 25, 2020

ASKOFU SANGU AENDESHA IBADA MKESHA KRISMASI....ATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI
Askofu wa Kanisa la Roman Katoliki jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu awali akiingia kanisani kwa ajili ya kuendesha Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas.
Na Marco Maduhu | Shinyanga | ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu, amewataka Watanzania kudumisha amani ya nchi ili waishi kwa upendo, utulivu, na kufanya shughuli za maendeleo.
Askofu Sangu amebainisha hayo jana wakati akiendesha Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Krismasi, iliyofanyika usiku kwenye Kanisa kuu la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Alisema watanzania wanapaswa kuilinda amani ya nchi, ambayo iliasisiwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuacha kuichezea ili kutoingia kwenye machafuko.
“Nawaomba watanzania tuidumishe amani ya nchi yetu, bila amani hakuna upendo, furaha, wala maendeleo, na kuna mataifa yana wivu sana na Tanzania, na kutaka tufarakane ili kuvuruga amani tuliyonayo, tusikubali bali tuilinde na kuidumisha amani ambayo tuliachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,” alisema Sangu.
Katika hatua nyingine Askofu Sangu aliipongeza Serikali mkoani Shinyanga kwa kupunguza tatizo la mauaji ya vikongwe, na kuomba kasi iongezwe zaidi kumaliza kabisa mauaji hayo ya watu wasio na hatia, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo bado yanaendelea.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alimuahidi Askofu Sangu kuwa maombi yake yote ambayo ameyaomba kwa Serikali yatatekelezwa, huku akiwataka wananchi wawe na hofu ya Mungu na kutenda yaliyo mema na kuacha kufanya mambo maovu, pamoja na kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu, akiendesha ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya KrismasI, katika Kanisa kuu la Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa salamu za Serikali, kwenye mkesha wa siku kuu ya Krismasi.
Waumini wakiendelea na ibada kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Ibada ikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wa kwanza kushoto), akiwa na waumini wakiendelea kusali kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Waumini wakitoa sadaka.
Waumini wakiendelea kutoa Sadaka.
Awali Askofu Sangu, akibariki waumini wakati akiingia Kanisani kuendesha Ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Askofu Sangu akibariki waumini kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya sikukuu ya Krismasi.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya sikukuu ya Krismasi.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Rais Magufuli Asali Krismasi Chamwino, Awataka Watanzania Kumshukuru Mungu Kuwaepusha Na Korona
Older Article
KATIBU MTENDAJI WA BASATA GODFREY MNGEREZA AFARIKI DUNIA
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment