Friday, December 25, 2020

NMB MASTABATA SIYO KIKAWAIDA - 12 WAONDOKA NA ZAWADI BAB KUBWA!
Benki ya NMB imewazawadia washindi 12 zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya milioni 28 kwenye bahati nasibu ya mwezi wa 12.
NMB kupitia kampeni yake ya ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ imewazawadia washindi hao zawadi ikiwamo simu janja, Runinga za kisasa, na Jokofu ambapo kila msindi alipatiwa zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kila mmoja.
Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi, Meneja wa Benki hiyo tawi la Mlima City, Irene Masaki alisema dhumuni la kampeni hiyo ni kuwahamasisha wateja kutumia kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa au huduma kupitia mtandaoni.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mliman City - Irene Masaki akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya "MastaBata Siyo Kikawaida" ya mwezi wa 12 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Mkaguzi Kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha - Pendo Mfuru, Balozi wa NMB - Nancy Sumari, Meneja wa Benki ya NMB Kitengo cha Kadi - Sophia Mwamwitu na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara za Kadi wa NMB - Lupia Matta.
Balozi wa Benki ya NMB - Nancy Sumari, akimpigia simu mmoja wa washindi wa "MastaBata Siyo Kikawaida" wakati wa kuchezesha droo ya mwezi wa 12 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa wateja walioshinda zawadi hizo ni Happy Luka Pallangyo, Masunga Jasila, Francis Julian na Rose Marealle. Mchakato wa kuwapata washindi hao ulisimamiwa na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kuhahatisha Tanzania - Pendo Mfuru.
Promosheni hiyo ilizinduliwa Novemba mwaka huu na itamalizika Februari mwakani. Promosheni hiyo, inahamasisha utimiaji wa NMB Mastacard and Mastacard QR katika kufanya manunuzi bila ya kutumia pesa taslimu. Kila wiki na mwisho wa mwezi kuna droo zinafanyika na wateja kuendelea kishinda Zawadi mbalimbali. Wateja wanapaswa kufanya miamala yao kupitia kadi ya NMB Mastercard au QR mara nyingi wawezavyo ili kuongeza nafasi zaidi za kushinda.
Katika kipindi chote cha kampeni, NMB itakabidhi zawadi kwa washindi 40 watakaoshinda Sh. 100,000 kila wiki na washindi 12 watazawadiwa simu janja aina ya Samsung galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. milioni 2.4 kila mwezi.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
BLOGGER MAARUFU KUTOKA MAREKANI ATEMBELEA TANZANIA
Older Article
Dkt.Abbasi Atuma Salamu Kwa Watanzania Kuwa Maandalizi Ya Tamasha Yamekamilika
Taasisi za Ulinzi wa Mlaji zimetakiwa kushirikiana na FCC
Hassani MakeroMar 21, 2025Safari ya Mafanikio ya NHC na Miaka Minne ya Mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani
Hassani MakeroMar 20, 2025Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment