NCBA Benki Tanzania Yamteua Julius Konyani Kuwa Mkurugenzi Mtendaji - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 30, 2021

NCBA Benki Tanzania Yamteua Julius Konyani Kuwa Mkurugenzi Mtendaji


Benki ya NCBA Tanzania imemteua Bwana Julius Konyani kuwa mkurugenzi mtendaji kwenye bodi ya wakurugenzi baada ya Gift Shoko kuhamishiwa Kenya kama Mkurugenzi wa Group pamoja matawi ya benki hiyo Afrika Mashariki. Uteuzi huu umethibitishwa na Benki Kuu ya Tanania (BoT).

Konyani anashika nafasi hiyo mpya akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 17 kwa bodi ya benki hiyo akiwa amefanya kazi na kushika nyadhifa mbali mbali za kiuongozi na kiutawala kwenye benki kama CRDB Bank PLC, NMB PLC, United Bank of Africa (T) limited.

Kabla ya uteuzi huo, Konyani alikuwa ni mkuu wa kitengo cha huduma za reja reja na za kibiashara za benki NCBA na amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza biashara za reja reja za benki hiyo kufuatia muunganiko kati ya NIC na Commercial Bank of Africa (CBA) mwaka 2019. Konyani aliongoza timu iliyoshughulikia muunganiko kati ya NIC na CBA ambao ulipelekea kuzaliwa kwa benki ya NCBA mwezi Julai mwaka 2020.

Konyani ana shahada ya uzamili kwenye biashara na ujasiriamali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia ni mwanachama hai wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS). Pia ni Mkurugenzi aliyethibitishwa wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT)

Akizungumzia uteuzi huo, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa NCBA Bank Tanzania Vinoo Sumaiya alisema uzoefu mkubwa wa Konyani utasaidia sana kuhakikisha benki inaendelea kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma hasa kipindi hiki ambacho benki hiyo inatekeleza mkakati wake wa kukuza biashara kupitia uvumbuzi na teknolojia.

Bodi inapenda kumpongeza Bwana Konyani kwa uteuzi huu. Nikiwa nimeshakutana na kufanya kazi na Konyani katika nafasi yake kabla ya uteuzi, nakiri umahiri wake katika utendaji na ninaamini atasaidia sana katika kukuza biashara ya NCBA Bank Tanzania katika ngazi ya bodi,” alisema Sumaiya.

Kwa upande wake Bwana Konyani alisema “Ninayofuraha kujiunga na bodi na pia nianyofuraha kuendelea kusukuma mbele ukuaji wa benki ya NCBA katika nafasi hii mpya. Naamini kuwa kufanya kazi pamoja na watu wengine ndani ya bodi benki ya NCBA itaendelea kuwa moja kati ya wadau muhimu kwenye sekta ya fedha hapa nchini na Afrika Mashariki,

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages