UNAMJUA MTU ALIYECHORA RAMANI YA MISIKITI MIWILI MITAKATIFU (Makka na Madina) - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 15, 2021

UNAMJUA MTU ALIYECHORA RAMANI YA MISIKITI MIWILI MITAKATIFU (Makka na Madina)


Na Mkeremi Jr Mkeremi | Alikuwa mhandisi na Msanifu wa Misri ambaye alipendelea kukaa mbali na umaarufu wa umma, Hajulikani na watu wengi:

Dk Muhammad Kamal Isma’eel (1908 - 2008)

Alikuwa ndio mtu mdogo zaidi kabisa katika historia ya Misri kumaliza kidato Cha Juu Shule ya Sekondari (cheti), mdogo kabisa kuingia katika Chuo cha Uhandisi cha Royal na pia mdogo kuhitimu, mdogo kupelekwa Ulaya kupata digrii tatu za udaktari katika Usanifu wa Majengo ya Kiislamu.

Alikuwa pia mdogo zaidi kupata skafu ya "Nile" Cha kiwango cha "Iron" kutoka kwa mfalme.
Alikuwa mhandisi wa kwanza ambaye alifanya upangaji na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa misikiti wa (Haramain) Makkah na Madinah.

Alikataa kupokea malipo yoyote kwa kazi yake hiyo ya uhandisi na usimamizi wa usanifu, licha ya juhudi za King Fahad na Kampuni ya Bin Laden.

Aliporudisha hundi ya mamilioni alimwambia Bakar Bin Ladan:

"Kwa nini nipokee pesa (kwa kazi yangu) katika misikiti miwili mitakatifu, nitamkabili vipi Mwenyezi Mungu (Siku ya Kiyama?)."


Alioa akiwa na miaka 44, mkewe akazaa mtoto wa kiume, na akafariki . Na baada ya hapo alibaki bila kuoa tena na akIjitolea muda wake wote katika kumwabudu Mwenyezi Mungu mpaka alipokufa.

Aliishi zaidi ya miaka mia moja ambayo alitumia katika kuhudumia misikiti miwili mitakatifu, akijiweka mbali na umaarufu wa media na umaarufu wa pesa.

Mwerevu huyu ana hadithi ya kushangaza kuhusu Kazi kwenye Haram Shareef (msikiti Mtakatifu wa Makka) alitaka kuweka Maru Maru( Mables)kwenye sakafu ya msikiti wa Haram pale panapofanyiwa 'tawaf'. Ilikuwa ni marumaru Maalum Meupe kwa ajili ya kuzuia joto.


Marumaru hii ilipatikana katika mlima mdogo huko Ugiriki.

Alisafiri kwenda Ugiriki na akasaini mkataba kununua kiasi cha kutosha kwa ajili ya haram (marbling) ambayo ilikuwa ni karibu nusu ya mlima.

Alitia saini makubaliano hayo na kurudi (Makkah) alifanikiwa kupata Marumaru kiasi ya Cha kutosha na kazi ilikamilika.


Baada ya kupita miaka 15, serikali ya Saudia ilimuita kuweka aina ya marumaru kama ile ya Maru maru katika msikiti Mtakatifu wa Madinah.

Mhandisi Muhammad Kamal alisema, Wakati Mfalme aliponitaka niweke Maru Maru kama ile katika msikiti wa Mtume, nilichanganyikiwa sana, kwa sababu kulikuwa na sehemu moja tu duniani inayopatikana aina ile ya marumaru, na ilikuwa ni Ugiriki, na tayari nilishanunua nusu ya ule Mllima.

Kamal alisema kuwa alikwenda kwenye kampuni ile ile huko Ugiriki na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji, na kumuuliza juu ya idadi iliyosalia.

Mkurugenzi Mtendaji alisema kwamba ilikuwa imeuzwa mara tu baada ya wewe kuondoka miaka 15 iliyopita. Kamal alihuzunika sana.


Kamal aliondoka kwenye mkutano na wakati anatoka ofisini kwao, alikutana na Sekreatari wa Ofisi na kumuuliza kama anaweza kukumbuka ni nani aliyenunua kiasi kile kichobaki Cha Maru Maru?

Alijibu kuwa itakuwa ngumu kujua mpaka kwenye rekodi za zamani.

Kwa ombi la Kamal, aliahidi kutafuta katika rekodi za zamani.

Kamal alimpa anwani na nambari ya hoteli, na akaahidi kumtembelea tena siku inayofuata.
Kamal alijiuliza wakati anatoka Ofisini, ni ; kwanini nataka kujua ni nani aliyeinunua?

Alijijibu Mwenyewe , Mwenyezi Mungu huenda akafanya jambo la ajabu litokee.

Siku iliyofuata, masaa machache kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege, Kamal alipokea simu kutoka kwa katibu akisema kwamba amepata anwani ya mnunuzi.

Kamal alienda ofisini kwao kwa mwendo wa polepole akifikiria atafanya nini na anwani ya mnunuzi, Wakati ni miaka mingi ilikuwa imepita?

Kamal alifika ofisini na Sekretari akampa anwani ya kampuni iliyonunua marumaru yote.

Kamal alisema kuwa moyo wake ulipiga kwa kasi pale tu alipogundua kuwa kampuni iliyonunua marumaru hiyo ilitoka Saudia.


Kamal alisafiri kwenda Saudi Arabia siku hiyo hiyo na alipofika, alienda moja kwa moja kwenye ofisi ya kampuni iliyonunua Marumaru yale na kukutana na Mkurugenzi wake, na kumuuliza kama alitumia yale marumaru aliyonunua miaka mingi iliyopita kutoka Ugiriki.

Alisema, siwezi kukumbuka.

Aliwasiliana na wake wa stoo na kuwauliza juu ya marumaru nyeupe kutoka Ugiriki na wakamwambia kwamba mzigo wote upo kama ilivyo na haukutumika kamwe.

Kamal alianza kulia kama mtoto mchanga, na akazidi kusimulia hadithi kamili kwa mmiliki wa kampuni hiyo.

Kamal alimpa mmiliki hundi tupu, na akamwuliza aandike kiasi anachotaka.

Wakati mmiliki alipogundua kuwa marumaru ni kwa ajili ya msikiti wa Mtume Mtukufu, alisema sitakubali hata Riyal (hela ya Saudia) moja.

Mwenyezi Mungu alinifanya ninunue hii marumaru na kisha nikizisahau kusudi zije kutumika kwa ajili ya msikiti wa Mtume Mtukufu.

Mwenyezi Mungu Amuweke Kamal mahali pa Juu kabisa katika 'Jannah' - Ameen.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages