BENKI YA EQUITY (T) YAPIGA JEKI MKUTANO WA WAKANDARASI (CRB) - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 27, 2021

BENKI YA EQUITY (T) YAPIGA JEKI MKUTANO WA WAKANDARASI (CRB)

Waziri wa Ujenzi Mh. Eng. Dr. Leonard Chamuhiro akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Mkuu wa Masoko wa Benki ya Equity(T) Godwin Semunyu. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimba na viongozi wa taasisi hizo.

Benki ya Equity (T) leo imekabidhi mchango wa Shilingi milioni 10 kwa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB), ili kufanikisha Mikutano ya Mashauri ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini mwaka 2021.


Akizugumza baada ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Mheshimiwa Waziri Chamuhiro, Mkuu wa Masoko wa Benki ya Equity Godwin Semunyu amesema kuwa Benki ya Equity ni mdau mkubwa wa sekta ya ujenzi nchini hivyo imeona umuhimu wa kudhamini mkutano huo ili kuwakutanisha wadau wote wa sekta hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu na hivyo kuongeza tija.

Equity Bank imejipanga kuendelea kutoa huduma nafuu za kifedha kwa wakandarasi wa ndani ili kuwaongezea mitaji na hivyo kuwapa uwezo wa kushindana sokoni. Nichukue fursa hii kuwakaribisha wakandarasi wote nchini kutembelea matawi yetu ya Benki ya Equity ili wafurahie huduma bora na nafuu zaidi sokoni” alisema.

Maofisa wa Benki ya Equity
Waziri wa Ujenzi Mh. Eng. Dr. Leonard Chamuhiro akisaini kitabu cha wageni katika banda la Benki ya Equity katika mkutano huo. Kushoto ni Innocent Ndika Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya Equity.

Benki ya Equity pia imeandaa sehemu maalum katika jengo la Daimond Jubilee ambapo mkutano huo unafanyika, ili kutoa maelezo ya bidhaa zake kwa washiriki wa mkutano huo.





No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages