Dar es Salaam, 24 Mei 2021 | Kampuni ya Facebook kwa ushirikiano na Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) wamezindua kipengele cha kuchangia damu nchini Tanzania. Kipengele hiki kitasaidia kuunganisha NBTS na kanda zake saba za kuchangia damu zinazopatikana sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Kipengele cha Facebook cha kuchangia damu kinalenga kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa kumsaidia mtu yeyote nchini Tanzania mwenye umri wa miaka 18-65 kujiandikisha ili wapate taarifa muhimu kuhusu maeneo ya kuchangia damu yaliyo karibu. Kipengele hiki pia kinawaruhusu watu kuwaalika ndugu na jamaa ili wajiandikishe kwenye huduma ya kupata taarifa muhimu kuhusu uchangiaji damu.
Tangu ilipoanzishwa mwaka 2004, Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama nchini Tanzania (NBTS) imetekeleza mageuzi ambayo yameisaidia kuacha mfumo wa kutegemea wachangiaji wa damu ambao 80% walikuwa ndugu wa mgonjwa, na kuanza kutumia mpango wa kusimamia uratibu wa wachangiaji hiari wa damu na wasiolipwa. Kwa mujibu wa takwimu za NBTS, vijana na wanafunzi nchini Tanzania ndio sehemu kubwa ya wachangiaji wa damu kwa sababu ni 80% ya damu yote nayochangiwa humu nchini. Kuzinduliwa kwa kipengele hiki cha kuchangia damu kutawasaidia watumiaji wa Facebook kuunganishwa na vituo vya kuchangia damu vinavyopatikana sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumzia uzinduzi huu, Mkuu wa Sera ya Facebook Kanda ya Afrika Mashariki na Upembe wa Afrika, Bi. Mercy Ndegwa, amesema, “Tuna furaha kubwa sana kuzindua kipengele hiki cha kuchangia damu nchini Tanzania na kitsaidia Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama nchini Tanzania katika kutimiza dhamira yake ya kuhakikisha upatikanaji wa damu nchini Tanzania. Facebook imejitolea kujenga jamii salama na zinazoshirikiana na ndio sababu tumeshirikia na NBTS katika kuzindua kipengele hiki ili kiwasaidie katika kuleta ufanisi kwenye uchangiaji damu nchini Tanzania.”
Kipengele cha Kuchangia Damu kilicho kwenye Facebook kina sehemu mbili:
● Kujiandikisha ili kupata taarifa — Watumiaji wa Facebook wanaweza kujiandikisha ili wapate taarifa kuhusu vituo vya kuchangia karibu vinavypatikana maeneo ya karibu.
● Hifadhi za Damu huhamasisha watu kuchangia damu - Vituo vya kuchangia damu vitashirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama ili kuwapata wachangiaji damu wanaweza kuchapisha kwenye ukurasa wao ili kuwahabarisha wachingiaji kuhusu mahitaji yao na kuweka kitufe cha kupiga simu kinachowawezesha wachangiaji damu kuwasiliana na nao moja kwa moja kutoka kwenye chapisho lao.
Tangu kipengele cha Kuchangia Damu kilipozinduliwa Oktoba 2017, zaidi ya watu milioni 85 wamejiandikisha kwenye huduma ya kupata taarifa kutoka kwenye hifadhi za damu zilizo maeneo ya karibu sambamba na fursa za kuchangia damu katika nchi zaidi ya 30. Tanzania inakuwa nchi ya 13 barani Afrika ambapo kipengele hiki kimezinduliwa.
Kinavyofanya kazi:
Watu wenye umri wa miaka 18 - 65 nchini Tanzania wanaweza kujiandikisha kwenye Facebook kama wachangiaji damu kwa kutembelea sehemu ya Uchangiaji Damu kwenye sehemu ya Kuhusu ya wasifu wao au wanaweza kutumia kiungo hiki: facebook.com/donateblood
No comments:
Post a Comment