Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu wa kuokoa maisha, Benki ya Akiba imeshiriki kikamilifu katika zoezi muhimu la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya siku ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambapo kilele cha maadhimisho yake ni June 14, 2021.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Benki ya Akiba, Dora Saria amesema jumla ya wafanyakazi takribani 30 kutoka Benki hiyo wamejitolea kushiriki katika zoezi la kuchangia damu kutokana na umuhimu wa zoezi husika, ili kuunga mkono jamii.
“Benki ya Akiba imekuwa mshiriki mahiri katika masuala ya kijamii kwa kutoa misaada katika sekta za Elimu, Mazingira na Afya kama ambavyo siku ya leo tumeshiriki katika zoezi hili kuchangia damu”, amesema Dora.
Pia kwa niaba ya Benki hiyo, Dora amesema wanatoa rai kwa Taasisi nyingine mbalimbali na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi hilo kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenye uhitaji wa damu.
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa kwenye maandalizi kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Baadhi ya Wananchi wakiendelea na Zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es Saalam kuelekea kilele cha maadhimisho June 14, 2021.
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akipima damu kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakipima kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Afisa Mauzo wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC ACB, Elizabeth Masolwa (kushoto), akiwa sehemu rasmi na mtaalam wa utoaji na uchangiaji damu.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria (kushoto), akitambulishwa kwa mtaalamu wa kutoa damu na mchangiaji wa damu Masoud Kipanya wakati wa zoezi la kutoa na kuchangia damu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment