Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia: Neno Lake la Mwisho – “KESHENI MKIOMBA” - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, June 6, 2021

Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia: Neno Lake la Mwisho – “KESHENI MKIOMBA”


Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua, maarufu kama TB Joshua amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 57.

TB amefariki saa chache baada ya kumaliza Huduma ya kichungaji katika Kanisa lake Jijini Lagos.

TB Joshua ni mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel, amelala mauti jijini Lagos Jumamosi jioni muda mfupi baada ya kumaliza programu kanisani kwake, taarifa hizi zilipatikana kutoka kwa vyanzo vya familia ambao hawakutaka kunukuliwa kama taarifa rasmi na baadaye kuthibitishwa kupitia Ukurasa Rasmi wa Instagram wa TB Joshua @tbjoshua asubuhi ya leo.

Sababu ya kifo haikufunuliwa mara moja, lakini vyanzo vya familia vilisema mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na uchunguzi wa mwili unaendelea.

Prophet TB Joshua ametumika kwa miongo kadhaa kama mhubiri mkali kwenye runinga, akitumia jukwaa lake kuvutia idadi kubwa ya Wakristo kutoka kote ulimwenguni, na Emmanuel TV, iliyoendeshwa nae, ni mojawapo ya vituo vikubwa vya utangazaji vya Kikristo vya Nigeria, vinavyopatikana ulimwenguni kupitia visembusi mbalimbali na satellite ulimwenguni kote.

Mnamo mwaka 2014, Kanisa lake lilikuwa katikati ya uchunguzi wa kitaifa kufuatia sehemu ya makao makuu ya Kanisa lake huko Lagos kuanguka, na kuwaacha watu kadhaa wakiuawa na wengine wengi kujeruhiwa. TB Joshua alikanusha madai ya uzembe na kesi juu ya tukio hilo bado unaendelea.

Sisi Wor’Out Media tunaungana na wananchi wa Nigeria, huduma ya SCOAN duniani kote pamoja na Emmanuel TV katika kipindi hiki kigumu! Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa! Jina la Bwana lihimidiwe!

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages