RC MAKALLA AHIMIZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, August 7, 2021

RC MAKALLA AHIMIZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI






Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
  • Asema Mazoezi muhimu kipindi hiki Cha Corona na Magonjwa yasiyoambukiza.
  • Ashiriki Mazoezi na kusaidia Vifaa vya mpira kwa Timu ya Masaki anayoifundisha na kuichezea.
  • Ahaidi kuifunga Azam Media Jumamosi ijayo Katika Uwanja wa Jeshi Masaki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa msaada wa Vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Jezi, Mpira na Vifaa vya kufundishia kwa Timu ya mpira wa Miguu ya Masaki akiwa Kama Mlezi na kocha wa timu hiyo.

Akizungumza wakati wa Mazoezi na Timu hiyo, RC Makalla amewahamasisha Wananchi kufanya Mazoezi ili kuimarisha Afya zao na kukabiliana na Magonjwa hususani Corona.

Aidha RC Makalla amesema akiwa kama Mlezi amedhamiria kuipandisha Daraja timu ya Masaki na kuhakikisha inashiriki michuano mbalimbali na ligi za ngazi ya juu ambapo kutakuwa na Timu ya *Masaki Vijana na Masaki Veterans.

Pamoja na hayo, RC Makalla amesema August 14 ya Timu ya Masaki inatarajia kushuka dimbani kuikabili timu ya Azam media ambapo amejinasibu kuigaragaza Timu ya Azam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages