VUNJO-MOSHI: NJIA PANDA RASMI KUHUDUMIWA NA MAMLAKA YA MAJISAFI MOSHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, August 15, 2021

VUNJO-MOSHI: NJIA PANDA RASMI KUHUDUMIWA NA MAMLAKA YA MAJISAFI MOSHI


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) itaanza kutoa huduma zake katika eneo la Njia panda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA Mhandisi Kija Limbe amesema hayo akiongea na Wafanyakazi wa Iliyokuwa Jumuiya ya watumia Maji Kilema Kusini na Bodi ya Maji Kirua Kahe Mtiririko iliyokuwa inatoa huduma eneo la Kata ya Njia Panda.

MUWSA inachukua Kata ya Njia Panda ambayo inaundwa na vitongoji vinne vya Njia Panda Mashariki, Njia panda Magharibi, Darajani na Faru.

Vitongoji vya Njia Panda Magharibi, Faru na Darajani vilikuwa vikihudumiwa na Jumuiya ya watumia maji ya Kilema na Kitongoji cha Njia Panda Mashariki kilikuwa kikihudumiwa na Bodi ya Maji Kirua Kahe Mtiririko.


Tukio hili ni mwendelezo wa makabidhiano ya eneo hilo lililokuwa likihudumiwa na jumuiya, na linazingatia Tangazo la Serikali Namba 113 la mwaka 2016.

Makabidhiano yalihusisha Menejimenti ya MUWSA, RUWASA Mkoa na RUWASA Wilaya.


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages