
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na mwandaaji wa filamu ya Royal Tour na Baadhi ya Wafanya Biashara wa Nchini Marekani baada ya Futari Jijini New York Marekani.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Wadau Wakuu wa Sekta ya Habari wa nchini Marekani katika Jiji la New York leo tarehe 18 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mtangazaji Maarufu wa Kituo cha Television cha CBS nchini Marekani Bi. Gayle King wakati alipokutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Wadau Wakuu wa Sekta ya Habari wa nchini Marekani katika Jiji la New York leo tarehe 18 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa US African Development Foundation USADF Travis Adkins wakati alipokutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Wadau Wakuu wa Sekta ya Habari wa nchini Marekani katika Jiji la New York leo tarehe 18 Aprili, 2022.
Saa chache kabla ya kuzinduliwa rasmi filamu ya Royal Tour ya Tanzania tayari mwanga na manufaa yake yameanza kuonekana ambapo wafanyabiashara na watu wengine mashuhuri walioona vipande vya awali vya filamu hiyo na kuvutiwa leo wamekutana na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye klabu ya faragha ya Lotos hapa New York, miongoni mwa waliohudhuria ni Meya mashuhuri wa jiji la New York, Eric Adams, ambaye ameeleza kuipenda Tanzania na kuahidi kuitangaza zaidi katika jiji lake la New York.
Mtu mwingine mashuhuri aliyehudhuria ukiondoa mabilionea na wamiliki wa makampuni makubwa duniani ikiwemo watangazaji wa CNN, CBS nk alikuwa ni Gayle King mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya CBC Mornings na “King in the House”
Gayle kwa hapa Marekani ni mtu mashuhuri akijulikana pia kwa urafiki wake wa karibu na wa miaka mingi na nguli mwingine Oprah ambako pia yeye Gayle ni Mhariri wa jarida la Oprah la O Magazine!
Jioni hii na usiku wa manane kwa saa za Tanzania, Rais Samia ataizindua filamu hiyo katika ukumbi wa Guggenheim Museum New York.
No comments:
Post a Comment