
Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Mapinga TotalEnergies, Jackson Swai, mkewe Joyce Swai, Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania, Jean Francois Schoepp, na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifurahia baada ya kufunguliwa kwa kituo hicho.

Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Mapinga TotalEnergies, Jackson Swai (kushoto) na mkewe Joyce Swai pamoja na na Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania, Jean Schoepp, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo hicho, Mapinga, Bagamoyo.
- TotalEnergies yahaidi kendelea kutoa huduma bora na salama
KAMPUNI kinara ya Mafuta nchini TotalEnergies imeendelea kuwafikia watanzania wenye malengo ya kumiliki vituo vya mafuta kwa kuzindua kituo kipya cha mafuta kinachomilikiwa na kuendeshwa na mtanzania Jackson Swai katika eneo la Mapinga, Bagomoyo mkoani Pwani kwa kupitia programu ya umiliki na uendeshaji (DODO) huku ikielezwa kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania pamoja na kushirikiana nao katika uwekezaji wa sekta hiyo ili kujenga uchumi imara.
Akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania Jean Francois Schoepp amesema, mahusiano hayo ni hatua kubwa katika kuendeleza soko la mafuta nchini na ni fursa kwa watanzania wenye maeneo na ndoto ya kumiliki vituo vya mafuta kuitumia program ya DODO yenye uhakika wa soko, mapato pamoja utambuzi kupitia chapa (brand) ya TotalEnergies yenye kutoa huduma bora na salama ikiwemo za mafuta bora (excellium fuel) na vilainishi.
Amesema TotalEnergies inathamini mchango na ushirikiano kutoka kwa wateja wao kupitia huduma na bidhaa wanazotoa, wanawakaribisha wawekezaji wengi zaidi na watapokea maoni ya watanzania ili kuendelea kuboresha huduma wanazozitoa.
Pia amempongeza mmiliki na mwendeshaji wa kituo hicho kwa kuiamini TotalEnergies nakueleza kuwa katika uzinduzi huo wateja watapata punguzo la shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta watakayonunua katika kituo hicho.
Kwa upande wake mmiliki na mwendeshaji wa kituo hicho Jackson Swai amesema, amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na kampuni ya TotalEnergies kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa na ubia huo wa kufanikisha uzinduzi wa kituo hicho utanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo kwa huduma za mafuta na vilainishi, bidhaa kupitia duka la Bonjour pamoja na ajira kwa wakazi wa maeneo hayo.
''Nimekuwa na ubia na kampuni ya TotalEnergies kwa miaka kadhaa kama msambazaji wa vilainishi vya kampuni na sasa uhusiano wetu umekuwa kupitia DODO programu...Ninajivunia kumiliki kituo cha mafuta cha TotalEnergies na kuwa sehemu ya kituo kinachoaminiwa na wateja nchini na dira yake ni kutoa huduma bora na salama.'' Amesema.
Swai amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi milioni 758 na elfu thelathini na sita na wataendeleza gurudumu la utoaji wa huduma bora kwa wateja na kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo ya uwekezaji ili kwenda sambamba na Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya uwekezaji.
Awali Meneja wa kuendeleza biashara kwenye vituo Adam Msangi amesema, kituo hicho kinachomilikiwa na mtanzania ni matokeo ya programu ya umiliki na uendeshaji Dealer Owns, Dealer Operate, (DODO) programu iliyobuniwa mahususi kwa wawekezaji wenye maeneo ya kujenga vituo vya mafuta vyenye leseni halali zilizotolewa na mamlaka ya Tanzania kuingia ubia na na kutumia chapa (brand) ya TotalEnergies.
Amesema kupitia DODO wawekezaji wananufaika na kutumia nembo ya TotalEnergies kampuni namba moja ya uuzaji mafuta na vilainishi nchini, soko la uhakika kote nchini ambako vituo hivyo vimesambaa.
Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wameeleza kufurahishwa na uwekezaji huo na kuwataka wawekezaji kutoka sekta mbalimbali kuwekeza katika Mkoa huo ambao una fursa nyingi za uwekezaji.
Katika uzinduzi wa kituo hicho wateja walipata zawadi mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata punguzo la shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta waliyonunua.

Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Mapinga TotalEnergies, Jackson Swai na Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania, Jean Francois Schoepp, wakiweka mafuta katika gari la mteja, wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Mapinga TotalEnergies, Bagamoyo, mkoani Pwani.

Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Mapinga TotalEnergies, Jackson Swai, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu ushirikiano na kampuni ya TotalEnergies, baada ya kufungiliwa kituo hicho, Mapinga, Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment