MELI ZA KIVITA KUTOKA CHINA ZAWASILI NCHINI KUADHIMISHA MIAKA 60 YA JWTZ NA USHIRIKIANO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, July 24, 2024

MELI ZA KIVITA KUTOKA CHINA ZAWASILI NCHINI KUADHIMISHA MIAKA 60 YA JWTZ NA USHIRIKIANO

Meli tatu za kivita za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China zikiwa katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo zimewasili leo Julai 24, 2024 zikiwa na wanajeshi kadhaa kwa ajili ya kushiriki mazoezi ya pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu kuadhimisho miaka 60 ya Jeshi hilo na ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na China tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY, Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Msemaji wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China Li Bo rank.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ujio wa Jeshi la Ukombozi wa Wau wa China.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Meli tatu za kivita za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China zimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa na wanajeshi kadhaa kwa ajili ya kushiriki mazoezi ya pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu maadhimisho miaka 60 ya Jeshi hilo na ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na China tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza leo Julia 24, 2024 katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akipokea Meli tatu za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY, Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan, amesema kuwa ujio wa meli hizo kutoka Jamhuri ya Watu wa China ni sehemu ya kuadhimisha ushirikiano wa miaka 60 kati ya Tanzania na China.

Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan amesema kuwa wakiwa nchini watashiriki mazoezi ya pamoja kati ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China kwa ajili ya kudumisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China ambapo tangu kuanzishwa kwake imefika miaka 60.

Amesema kuwa sio mara ya kwanza Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China kuja nchini Tanzania kufanya mazoezi ya pamoja na Jeshi la JWTZ kwani mwaka 2014, 2019, 2020 walikuja kushiriki mazoezi.

Ujio wa Jeshi la Ukombozi Watu wa China tutajifunza mbinu mbalimbali kutokana wao wameendelea zaidi katika masuala ya kijeshi” amesema.

Amesema kuwa mazoezi ya pamoja na Jeshi la Watu wa China watashiriki vikundi mbalimbali vya Jeshi la Ulinzi la Tanzania, huku akifafanua kuwa kupitia mazoezi hayo yatawasadia kuongeza uwezo wa kijeshi katika utekelezaji wa majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages