SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YATILIANA SAINI UJENZI WA MRADI WA UMEME WA JUA MAKUNDUCHI ZANZIBAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, August 28, 2024

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YATILIANA SAINI UJENZI WA MRADI WA UMEME WA JUA MAKUNDUCHI ZANZIBAR

Waziri wa Maji Nishati na Madini Shaib Hassan Kaduwara (aliyesimama kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Joseph Kilangi wakishuhudia Utiaji Sani Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Jua katika Kijiji cha Makunduchi Zanzibar baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Potential Builders Ltd kutoka Daresalaam ambapo zaidi ya Shiling Bilioni Tisa zinatarajiwa kutumika.kulia anaetia saini ni Meneja Mkuu Shirika la Umeme Haji Haji na mwengine ni Eng.David Mwasomola, hafla iliofanyika ofisi ya ZURA Maisara Zanzibar.
Meneja Mkuu Shirika la Umeme Haji Haji (mwenye koti) akipeana mikono na kubadilishana hati za Saini na Eng,David Mwasomola wa Kampuni ya Potential Builders Ltd kutoka Daresalaam katika hafla ya Utiaji Saini baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni hio kuhusiana na Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Jua katika Kijiji cha Makunduchi Zanzibar ambapo zaidi ya Shiling Bilioni Tisa zinatarajiwa kutumika.hafla iliofanyika ofisi ya ZURA Maisara Zanzibar.

Na Ali Issa na Najjash Ubwa - Maelezo Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Imetiliana saini ya ujenzi wa Miundo mbinu ya Mradi wa umeme wa Jua kati yake na Kampuni ya Potential Builders Limited kutoka Tanzania Bara.

Utiaji wa saini huo ulifanyika huko Maisara katika jengo la ZURA kwa upande wa Serikali aliesaini mradi huo alikuwa ni Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Haji Haji na kwa upande wa kampuni hio alikuwa Engineer David .A. Mwasomola.

Akitoa pongezi zake Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe, Shaibu Hassan Kaduwara alisema kumalizika kwa mradi huo umekuja kufuatia kukatika katika kwa umeme hivyo mradi huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hio katika visiwa vya Zanzibar.

Alisema kuwa itakuwa vyema mradi huo ukamalizika kabla ya miezi sita ya makubaliano.

Aliitaka Kampuni hio kufanya kazi Usiku na Mchana ili kumalizika mradi kwa wakati.

Aidha alilitaka Shirika la Umeme kuwa kribu na kampuni hiyo kwa usimamizi na ufatiliaji mwenendo mzima wa ujenzi.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi Alisema Mradi huo unajengwa kwa pesa za mkopo kutoka Benki ya Dunia na utakaogharimu zaidi ya shiligi Bilioni 9 ambao ujenzi wake utaanzia usafishaji wa maeneo ujenzi wa barabara za ndani na sehemu za kuhifadhia mitambo.

Alisema Umeme huo wa Megawatts 18 utajengwa katika maeneo ya Makunduchi Mkoa wa kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages