RC CHALAMILA ATOA SALAAM ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2025 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, December 23, 2024

RC CHALAMILA ATOA SALAAM ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2025

Kuelekea sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amesema ulinzi na usalama umeimarishwa ili kuhakikisha wananchi hususani wakazi wa Mkoa huo wanakuwa salama katika kipindi chote cha sikukuu na baada ya sikukuu, pia amewataka wazazi na walezi kusimamia vema usalama wa watoto kwa kutowapeleka kwenye maeneo hatarishi.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Disemba 23, 2024 katika Hotel ya Johari Rotana jijini Dar es salaam wakati akitoa salamu za sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya amesema Mkoa kupitia jeshi la polisi umeimarisha ulinzi ambapo ameitaka jamii kushirikiana na serikali kudumisha amani ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla

Aidha Kupitia salamu hizo za sikukuu RC Chalamila amewatoa shaka wananchi wa Mkoa huo kuhusiana na miradi ya ujenzi wa barabara kupitia DMDP ambayo imeonekana kuchelewa ambapo amesema miradi hiyo imeshakabidhiwa kwa wakandarasi na inatarajia kuanza mapema januari mwaka 2025 huku pia akieleza mipango ya kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji safi.

Vilele RC Chalamila amezungumzia mkakati wa kuanza kwa shughuli za kibiashara saa 24 eneo la Kariakoo ambapo amesema zoezi hilo litazinduliwa rasmi mwezi januari 2025 ambapo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na maafisa biashara wanapaswa kuainisha maeneo ambayo biashara zinaweza kufanywa saa 24 ikiwwmo eneo la kariakoo.

Sanjari na hayo Chalamila amezungumzia mikakati ya Mkoa huo kupokea wanafunzi wa chekechea, darasa la kwanza na kidato cha kwanza na kueleza kuwa serikali imeendelea kuwekeza fedha ili kufikia malengo ya elimu hivyo ambapo amehimiza wafanyabiashara kulipa kodi ili malengo hayo yaweze kutimia.

Mwisho akijibu maswali ya waandishi wa habari RC Chalamila ameeleza mipango ya kuboresha huduma za usafiri wa mwendokasi maarufu BRT ambao kwa sasa amesema idadi ya mabasi haitoshelezi, pia amehimiza madereva kutoingilia njia za mabasi ili kuepuka ajali na amesisitiza wananchi kutovamia maeneo kiholela kufanya biashara

Ifahamiki kuwa utaratibu huu wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa salamu za sikukuu za mwisho wa mwaka imekuwa na nafasi kwa mkuu wa mkoa kuelezea maendeleo ya mkoa huo na changamoto zilizopo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages