Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman (KULIA) akiondoa pazia kuweka jiwe la Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3, hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Na Rahma Khamis, Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haruon Ali Suleiman amewataka wananchi kuacha kujenga na kulima pembezoni mwa miundombinu ya barabara ili iendelee kudumu kwa muda mrefu.
Wito huo ameutoa huko Kidimni Wilaya ya Kati wakati akifungua barabara za ndani zilizo kamilika kujengwa kwa kiwango cha lami ya Kidimni - Ubago ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kuwa maendeleo hayana dini wala ukabila hivyo ni muhimu kuitunza vizuri barabara hiyo kwa kuzingatia miundombinu iliyowekwa sambamba na kuwataka vijana kuwa wazalendo na kuipenda Nchi yao ili kuendeleza Amani iliyopo nchini.
Akitoa taarifa ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Makame Machano Haji amesema jumla ya zaidi ya Dola za kimarekani (USD) milioni 80 zimetumika katika ujenzi wa barabara zote za ndani Unguja na Pemba zenye kilomita 275.9.
Aidha amefahamisha kuwa barabara hiyo imezingatia miundombinu yote muhimum kwa ajili ya matumizi ikiwemo njia ya kupitishwa Maji.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayuob Muhammed Mahmoud amesema ujenzi wa barabara hiyo ni maendeleo makubwa ndani ya Mkoa huo kwani umepata bahati ya kujengewa barabara za lami zenye kiwango kwa zaidi ya asilimia 70 hadi kufikia Sasa.
Nao baadhi ya wananchi wa eneo Hilo wamesema wamefarajika sana kujengewa barabara hiyo kwani itawasaidia katika harakati zao za kuleta maendeleo nchini sambamba na kuahidi kuitunza na kuitumia vyema miundombinu hiyo.
Ujenzi wa barabara hiyo umeanza Novemba 11 mwaka 2022 na kukamilika Disemba 15 ambapo kauli mbiu ya Mapinduzi ya mwaka huu Miaka 61 ya Mapinduzi Amani, Umoja Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman (KULIA) akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3, hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kisini Ayoub Mohamed Mahmoud na Viongozi mbalimbali wakitembea kwa Miguu baada ya Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3, hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa hotuba ya makaribisho kwa Wageni mbalimbali katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3, hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akizungumza katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3, hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
Baadhi ya wageni waalikwa na wananchi waliohudhuria katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Kidimni-Ubago Km 4.3,hafla iliofanyika Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakiwa na Kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi: Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu-Mapinduzi Daima."
No comments:
Post a Comment