TANESCO Yatoa Elimu Kuhusu Nishati Safi na Miradi ya Umeme Katika Mkutano wa Nishati wa Afrika - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, January 27, 2025

TANESCO Yatoa Elimu Kuhusu Nishati Safi na Miradi ya Umeme Katika Mkutano wa Nishati wa Afrika

Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, linashiriki katika Maonesho kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi wa Afrika (African Energy Summit) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Mkutano huo umeanza leo Januari 27, 2025 unawakutanisha Wakuu wa Nchi Barani Afrika kujadili mikakati ya upatikanaji wa nishati ambapo lengo kuu ni kuwafikishia nishati ya umeme Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

TANESCO kama mdau muhimu wa nishati ya umeme hapa nchini imeendelea kutumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wadau juu ya matumizi ya nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na maendeleo ya miradi ya umeme na matumizi ya nishati safi ya umeme kupikia.

Mkutano huo utamalizika kesho Januari 28, 2025 ambapo unatarajiwa kuonyesha mwelekeo wa mpya nishati katika bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages