Vijana wa vyuo na vyuo vikuu katika Mikoa yote Tanzania tumekuabaiana kusaini kwa saini zetu kitambaa chetu kuashiria kuwa tunakubaliana na Azimio la kumteua Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kuwa mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya CCM mwaka 2025-2030 na Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea Mwenza, na Dkt Hussein Ali Mwinyi kugombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM 2025-2030.
Wanavyuo katika Mikoa yote tunaendelea kuwasiliana kwa ukaribu sana ili Mikoa yote tuweze kusaini kitambaa hiki kwani tunamuunga mkono Dkt SAMIA SULUHU HASSAN na Dkt HUSSEIN ALI MWINYI.
Hayo yametanabaishwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati baada ya matembezi ya CCM yaliyofanyika katika Mkoa wa Morogoro.
WANAVYUO TUNA DENI NA DKT SAMIA SULUHU HASSAN!
No comments:
Post a Comment