
KATIBU wa idara ya uhusiano wa Kimataifa vyuo na vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg Emanuel Martine amekutana na wanavyuo na wanachama wa UVCCM vyuo na vyuo Vikuu kutoka mkoa wa Morogoro ikiwa ni shamrashamra kuelekea miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM.
Vijana wa vyuo na vyuo Vikuu mkoa wa Morogoro wamepata nafasi ya kujifunza historia ya CCM na kutembezwa katika jengo la UVCCM Taifa Dodoma ikiwa ni pamoja na kupata historia za viongozi waliopita, historia zao ndani ya UVCCM na mahali walipo kwasasa.



Mkuu wa idara ya Organization na siasa UVCCM Taifa Ndg Mrakib Mbaruk Mrakib amepata kuwaelezea historia hiyo ya Viongozi wa mwanzo wa UVCCM Taifa hadi sasa chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg Mohammed Ali Kawaida (MCC)
Wanavyuo wa vyuo na vyuo Vikuu wameahidi kuendelea kumuunga mkono Dkt Samia Suluhu Hassan na mgombea Mwenza Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi katika uchaguzi wa 2025 kwa kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo 2025, Kura za wanavyuo ni kwa Samia Suluhu Hassan na Balozi Emmanuel Nchimbi na Dkt Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.




No comments:
Post a Comment