SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA MASOKO ZAIDI ILI KUTOA FURSA PANA YA KUFANYA BIASHARA KATIKA MAZINGIRA MAZURI. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, February 25, 2025

SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA MASOKO ZAIDI ILI KUTOA FURSA PANA YA KUFANYA BIASHARA KATIKA MAZINGIRA MAZURI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wafanyabishara kuwa Serikali itaendelea kujenga Masoko zaidi ili kutoa fursa pana ya kufanya Biashara katika Mazingira mazuri.

Rais Dkt.Mwinyi ametoa Tamko hilo alipotembelea Masoko Ya Jumbi, Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia Mwenendo wa Biashara na Upatikanaji wa Bdhaa za Vyakula kuelekea Mwezi Wa Ramadhani.

Dkt.Mwinyi Ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa Ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine Maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye Biashara kwenye Mazingira rasmi.

Amewasisitiza Wafanyabishara kuepuka kufanya Biashara Barabarani na kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali hivi sasa.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuridhishwa na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei wakati Ramadhani Itakapoanza.

Kuhusu Suala la Usafi wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati Wote.

Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji na Vipooza hewa katika Masoko yote pamoja na kuimarisha Usafi.
Ziara hiyo ya Rais Dkt.Mwinyi ni ya Kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi, Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages