UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO MKOANI ARUSHA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, February 28, 2025

UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO MKOANI ARUSHA


TAARIFA KWA UMMA
UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO MKOANI ARUSHA

Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 08/03/2025 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha tutatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto.

Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote ambapo Wataalamu Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) watatoa huduma hii tarehe 01 - 08/03/2025 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha.

Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu ya lishe bora kwa wananchi itakayowapa uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanayoweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo na wale watakaokutwa na matatizo yatakayohitaji matibabu ya kibingwa watapewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunawaomba wanawake, wajawazito, wazazi na walezi wenye watoto wajitokeze kwa wingi kupima afya zao kujua kama wana matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa watakaogundulika kuwa wagonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754849850 na 0752211081.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Imetolewa na:
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages