MKUU wa Divisheni ya Rasilimali watu Utawala na Mipango ZEEA Pemba, Raya Mohamed Abdalla, akiwasilisha mada ya dhana ya ujasirimali, wakati wa mafunzo kwa wajasirimali wa Mkoa wa Kusini Pemba, ambao wameomba mikopo mbali mbali kutoka ZEEA.
BAADI ya Wajasirimali kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, wakifuatilia kwa makini Mfunzo mbali mbali kabla ya Mkopo, mafunzo hayo yametolewa na ZEEA.
Na Abdi Suleiman, Pemba
WAJASIRIAMALI Kisiwani Pemba, wameshauriwa kuomba mkopo kwa ajili ya matumizi walionayo na sio kwa mambo mengine, ambayo yatakayopelekea kushindwa kurudisha marejesho ya Mkopo huo.
Hayo yameleezwa na Afisa Mauzo na Mikopo kutoka benki ya TCB Ndg.Khamis Juma Khamis, wakati wa mafunzo kwa wajasirimali ambao tayari wameshaomba mikopo kupitia ZEEA, yaliofanyika katika Wilaya ya Mkoani na Wilaya ya Chake Chake.
Alisema mjasiriamali anapaswa kuomba Mkopo kulingana na mahitaji yake aliyonayo na sio kitu chengine, kwani atakua hajautendea haki mkopo huo, na kutokutimiza malengo ya serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi ya kuwainua wajasiriamali.
Alisema Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar chini ya Rais Dkt.Husein Ali Mwinyi, aliweza kutoa mitaji kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo, ili kujiendeleza kiuchumi na kukuza kipato chao.
Alifahamisha kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.Hussein Mwinyi, aliwaeza na kuwaunganisha na mabenki kwa lengo la kutoa mitaji hiyo kwa wajasimiali, hivyo wananchi na wajasiriamali waliowengi wanahitaji kujua umuhimu wa matumizi ya mkopo.
“Kama tunavyofahamu kwamba waliowengi wanaomba mikopo kwa ajili ya mahitaji yao na biashara zao zilivyo, ila walio wengi hawafahamu kama mkopo mtu anaomba kwa mahitaji yake aliyonayo na sio kwenda vyengine,” alisema.
Mapema akifungua mafunzo hayo afisa Mafunzo na miradi ya Uwezeshaji kutoka ZEEA Pemba Fatma Ali Salim, alisema ZEEA inamajukumu ya kimkakati kwa ajili ya kuwawezesha wananchi.
Alisema ZEEA ni taasisi iliyoundwa kisheria na kwa sheria namba 2/2022, taasisi ambayo inamajukumu ya kimkakati, ya kuwawezesha Wananchi Kiuchumi na nichombo ambacho Rais Dkt:Huseina Ali Mwinyi, alikiunda akiwa na matarajio makubwa kwa wajasiriamali na wananchi kuweza kujiinua kiuchumi.
Aidha alifahamisha kwamba ZEEA inamajukumu makubwa manne, ikiwemo jukumu la kuwajengea uwezo wajasiriamali, ili kupata ufanisi wa kuendeleza biashara zao wanazozifanya, pia wanahakikisha wajasirimali baada ya kuzalisha wanatafutiwa masoko na kuuza bidha zao kupitia maonyesho mbali mbali.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, mkuu wa Divisheni ya Rasilimali watu Utawala na Mipango ZEEA Pemba Raya Mohamed Abdalla, alisema uwepo wa masoko mbali mbali ya wajasirimali ni fursa kubwa kwao ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.
Nae Kaimu Mkuu Divisheni ya Mikopo na Mitaji ZEEA Pemba Haji Khamis Haji, alisema uwekaji wa kumbukumbu ni jambo la mtambuka na nirasilimali muhimu inayopaswa kuhifadhiwa kwa ajili ya baadae.
Kwa upande wao wajasirimali hao, wamesema mjasirimali siku zote ni mtu wa chini, hivyo waliomba kupatiwa elimu ya uhakika ili biashara zao ziweze kukua.
No comments:
Post a Comment