
Gavana wa Benki Kuu Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wkurugenzi ya Benki ya Selcom Microfinance Tanzania Limited, Leonard Mususa.
“Huduma Ya Kifedha Ya Kidigitali Yenye Makato Nafuu Kuliko”
11 Februari 2025, Dar es Salaam, Tanzania – Benki ya Selcom Microfinance Tanzania Limited imezindua rasmi huduma yake maridhawa ijulikanayo kama SELCOM PESA, huduma ya kifedha ya kidigitali ambayo imebuniwa mahsusi kubadilisha sekta ya kifedha nchini Tanzania.
Selcom Pesa ni huduma ya kifedha yenye kulenga na kuleta mabadiliko kwa kuwawezesha Watanzania kupata huduma za kifedha kuwa njia rahisi, salama, na nafuu. Selcom Pesa imekuja kuondoa changamoto zinazowakabili watumiaji wa fedha kwa njia ya mtandao. Katika kumjali kila mtanzania kufikiwa na huduma za kifedha Selcom Pesa yenye uwanda mkubwa wa kiteknolojia imebuniwa ili kuonyesha kwamba suala la kiteknolojia lipo ili kuleta unafuu wa huduma za kifedha na sio kuwa kisingizio kwa makampuni ya KIFEDHA ili kujipatia faidia kutokana na kuweka gharama kubwa za makato kwa watumiaji wa huduma hizo.
Wakizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Mheshimiwa Emmanuel Tutuba, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Selcom Bank, Mheshimiwa Leonard Mususa, ambapo wote walisisitiza umuhimu wa mapinduzi ya kidigitali ya kifedha nchini Tanzania. Uzinduzi wa SELCOM PESA ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhamasisha mageuzi ya kiuchumi na kidigitali nchini, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mwenyekiti wa Bodi alisema nafasi muhimu ya Benki Kuu katika kukuza mazingira ya kifedha yenye usalama, ushirikishwaji, na yanayotokana na teknolojia. Utambulisho wa Mfumo wa Malipo ya Haraka wa Tanzania (TIPS) ulisisitizwa kama mpango muhimu wa kurahisisha miamala ya kifedha, kuwawezesha Watanzania kufikiwa na miamala haraka, nafuu, na inayopatikana kwa wote. Huduma ya SELCOM PESA ni uthibitisho wa uwezo wa sekta binafsi kutumia mifumo hii, kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kifedha za ubora wa juu na gharama nafuu.
Katika hotuba yake, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alieleza kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika ushirikishwaji wa kifedha, huku kukiwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi wanaotumia huduma rasmi za kifedha. Hata hivyo, changamoto kama vile gharama kubwa za miamala na upatikanaji wa huduma bora za kifedha bado zinajitokeza, hususan miongoni mwa wananchi wa kipato cha chini. SELCOM PESA inalenga kushughulikia changamoto hizi kwa kutoa suluhisho za kifedha za nafuu, rahisi, na salama kwa Watanzania wote. Mheshimiwa Emmanuel Tutuba pia aliwataka watoa huduma wengine kuchukua fursa ya mipango ya serikali kama vile TIPS, ambayo inachangia kupunguza gharama za uendeshaji na kutoa huduma nafuu kwa wananchi wa kawaida.
Huduma ya SELCOM PESA imeunganishwa na jukwaa la TIPS, na kufanya kuwa mojawapo ya huduma za kifedha za kidigitali zenye gharama nafuu zaidi zinazopatikana leo, zikiwa na ada za miamala chini kuliko watoa huduma wengine. Wateja wanaweza kuipakua kupitia Google Play au Appstore na kufurahia miamala kama vile uhamishaji wa fedha kutoka benki kwenda mitandanoya simu, uhamishaji wa fedha kutoka mitandao ya simu kwenda benki au kutoka benki nyingine hadi Selcom Pesa, malipo ya bili na Malipo ya Serikali (GePG) n.k.

Uzinduzi wa Selcom Pesa umeenda sambamba na uzinduzi wa kampeni maalum ya masoko iitwayo 5 kwa Jero (Tano Kwa Jero). Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Microfinance ya Selcom Tanzania, Mheshimiwa Julius Ruwaichi alisema, hii ni mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo wateja wanapewa kifurushi cha kufanya miamala. Kampeni ya 5 kwa Jero itawapa fursa wateja wote wa Selcom Pesa kufanya miamala mitano kwa siku kwa ada ya Tsh 500 tu.
Katika kuhitimisha, Gavana alitoa pongezi za dhati kwa Benki ya Microfinance ya Selcom Tanzania na mshirika wake mkubwa, Selcom Paytech Limited, kwa uzinduzi wa mafanikio wa SELCOM PESA. Mpango huu unatarajiwa kutoa matokeo chanya kwa sekta ya kifedha na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa kidigitali wa Tanzania.

No comments:
Post a Comment