
Ifahamu jamii ya ndege wasafiri ambao husambaa katika kipindi cha kiangazi kwenye bara la ulaya, Asia na Afrika. Ndege hawa wanajulikana kama Cuckoo (ama Kekeo kwa Kiswahili).
Jamii hii ni aina ya ndege ambao hukwepa majukumu kwa kupandikizia watoto wao kwa jamii nyingine za ndege ili walelewe tangu yakiwa bado mayai. Kwa maana kuwa hutaga kwenye viota vya ndege wengine kisha wao huendelea kula maisha ya ujana bila kujali huko nyuma mambo yatakuwaje kwa hao walezi waliosingiziwa.
Pamoja na kuwa mayai yao huwa makubwa kuliko ya walezi wao, ndege hawa huakikisha sana yanaendana na mayai mengine waliyoyakuta kwenye viota vya walezi wao kwa ukubwa kiasi pamoja na rangi ili walezi hao wasistuke.


Mayai ya cuckoo yakiwa na mayai mengine ya walezi wake.
Chakula cha kawaida cha cuckoo kina jumuisha wadudu, nyungunyungu (caterpillars), ambao ni chakula cha ndege wengi duniani. Muda mwingine hula mayai na vifaranga wengine kwenye viota ili kujikidhi mahitaji yake.
Cuckoo kama jamii ya ndege Parasite; hutaga mayai yao kwenye viota vya ndege wengine.
.jpg)
Vifaranga vinavyototolewa huwasukuma vifaranga au mayai ya ndege mwingine nje ya kiota.
Cuckoo jike hutembelea hadi viota 50 tofauti tofauti kipindi cha utagaji.
Kikawaida cuckoo huanza kutaga baada ya miaka miwili.
Cuckoo jike wamepatiwa uwezo mkubwa wa kuweza kuigilizia miundo na rangi za mayai ya ndege wengine.
Inaelezwa kuwa Cuckoo dume huzaa na majike wengi na watoto wao hukuzwa na jamii zaidi ya moja ya walezi.

Kifaranga wa cuckoo hutotolewa baada ya siku 11-13. Njia hii ya utotolewaji haraka hutumiwa na jamii nyingi ya ndege vamizi.
Kifaranga cha cuckoo huwa mkubwa kimwili kuliko kifaranga wa ndege mlezi. Na hutaka kuudumiwa chakula pekee yake kutoka kwa wazazi walezi. Hivyo baada ya kutotolewa, husukuma mayai mengine nje; na endapo kuna kifaranga tofauti na yeye atabahatika kutotolewa mbele ya macho yake, naye hutupwa nje vilevile.
Baada ya siku 14 tangu kutotolewa kifaranga huyu wa cuckoo huwa mkubwa mara 3 zaidi ya mzazi mlezi.

Sababu haswa za cuckoo hawa makinda kutupa mayai mengine au vifaranga wengine wa mwenyeji wake nje ya nyumba; bado haifahamiki.
Ndege huyu anatufundisha kuwa kuna watu katika maisha yetu ya kila siku tunaishi nao lakini kwa namna moja au nyengine wanafanana na Cuckoo.
.jpeg)
No comments:
Post a Comment