DC NYUNDO AWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA UUZAJI ARDHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, November 22, 2025

DC NYUNDO AWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA UUZAJI ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, amewasimamisha kazi viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nanjirinji A, Kata ya Nanjirinji, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ugawaji na uuzaji wa ardhi kinyume cha utaratibu pamoja na matumizi mabaya ya mali za umma.

Baadhi ya wananchi wakiwasikiliza viongozi kutoka wilaya ya Kilwa.
Na Fredy Mgunda, Kilwa Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, amewasimamisha kazi viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nanjirinji A, Kata ya Nanjirinji, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ugawaji na uuzaji wa ardhi kinyume cha utaratibu pamoja na matumizi mabaya ya mali za umma.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wananchi kuwasilisha malalamiko mbele ya Mkuu wa Wilaya, wakimtuhumu Mwenyekiti Hamadi Makakala na Mtendaji Mbaruku Malukula kwa kufanya maamuzi makubwa bila kuwashirikisha wanajamii, kinyume na misingi ya utawala bora.

Akizungumza baada ya kusikiliza malalamiko hayo, DC Nyundo alisema kuwa ameunda kamati maalumu ya uchunguzi itakayopitia tuhuma hizo kwa kina na kutoa mapendekezo yatakayoiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki.

Hatutaacha mwanya kwa mtu yeyote kutumia madaraka vibaya au kudhulumu rasilimali za wananchi. Uchunguzi utafanyika kwa uwazi na hatua kali zitachukuliwa kulingana na matokeo,” alisema Nyundo.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa waangalifu dhidi ya taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, akiwataka kutegemea vyanzo vya uhakika ili kuepuka kupotoshwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Hemed Magaro, alitoa ufafanuzi kuhusu utofauti kati ya kuuza ardhi na kugawa ardhi kwa utaratibu maalumu, akisisitiza kuwa ardhi ya kijiji haiwezi kuuzwa bila kufuata sheria, taratibu na ridhaa ya mkutano mkuu wa kijiji.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages