MHE. MWINJUMA ATOA MSIMAMO WA SERIKALI MABADILIKO YA UENDESHAJI SIMBA SC - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, November 30, 2025

MHE. MWINJUMA ATOA MSIMAMO WA SERIKALI MABADILIKO YA UENDESHAJI SIMBA SC

Serikali imesisitiza kuwa haitalazimisha Klabu yoyote nchini kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji bila uamuzi wa wanachama wake, na kwamba jukumu lake kuu ni kuhakikisha mchakato wowote unaotekelezwa unaendana na Sheria za nchi pamoja na kanuni zinazoongoza mchezo wa mpira wa miguu.

Kauli hiyo imetolewa leo, Novemba 30, 2025, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Simba uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mwinjuma amesema kuwa, hatima ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo iko mikononi mwa wanachama, na Serikali haina dhamira ya kuingilia maamuzi yao.

Mchakato huu ni wenu; ni uamuzi wa wanachama. Kama mtakubaliana kuendelea, kutathmini upya au kubadili mwelekeo, basi uamuzi huo utaheshimiwa,” amesema Mhe. Mwinjuma.

Ameongeza kuwa, Serikali inatamani kuona mijadala na maamuzi kuhusu mustakabali wa klabu hiyo haitawaliwi na hisia bali busara, kuzingatia sheria, maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa michezo nchini.

Lengo letu ni kuhakikisha mjadala na maamuzi ya leo hayapotezi mwelekeo kutokana na hisia, bali yanaongozwa na busara, sheria, maslahi ya klabu na maendeleo ya michezo nchini,” amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages