BODI ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza
miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu
huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.
Agizo hilo limetolewa
na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) jana Jijini Dar es Salaam.
Profesa
Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa
miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika
bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.
“Inasikitisha
kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu
miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea
uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema
Profesa Ndalichako.
Ndalichako
ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na
kuwachukulia hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika ucheleweshaji wa
kuanza kwa miradi hiyo.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako kwa
kuwa muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa
baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku
akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.
“Mhe Waziri,
maelekezo yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na timu yangu
tutayafanyika kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana nawe wakati
wowote,” alisema Mduki.
Awali akisoma
maelezo mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi amebainisha changamoto
kadhaa katika eneo hili la utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwa ni
pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya elimu na
mafunzo ya ufundi akitolea mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo
wanakadiriwa kuwa laki sita kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA, VYA
Serikali na binafsi ni kati ya 125,000 tu kwa mwaka.
Bodi
iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria
Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi desemba 2016 alipoteuliwa
Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe 10 kutoka maeneo ya ujuzi
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment