Mama ongea na mwanao ni kampeni iliyoendeshwa kipindi cha
uchahuzi wa rais 2015, ambapo wasanii mbalimbali waliungana kupigania chama cha
Mapinduzi CCM, Steven Nyerere akisaidiana na Wema Sepetu wakiwa viongozi wa
kampeni hiyo walizungunguka nchi zima kupigania CCM kuendelea kuwa madarakani.
Katika kampeni hiyo kila msanii alihaidiwa kulipwa laki
tano mara baada ya kumaliza kuzunguka kila mkoa mmoja, lakini kwa baadhi ya
maelezo ya wasanii mara tu baada ya kumaliza mkoa mmoja hawakuweza kukabidhiwa
fedha zao walizoahidiwa kabla ya kampeni.
Utata umezuka katika wasanii walioshiriki kampeni ya mama
ongea na mwanao kwani wasanii hao wametengeneza tabaka wapo wanaodai kulipwa
fedha zao pia wapo wanaodai kutolipwa fedha zao.
Hivyo baadhi ya wasanii wameungana na kumtaka mchekeshaji
Steve Nyerere kuonesha mkataba wa malipo ambao ulitolewa na CCM lengo
kubwa ni kukata mzizi wa fitina baina ya wasanii, wananchi na uongozi mzima wa
CCM.
Pia wameomba Viongozi wa CCM kumbana Steve Nyerere, aeleze
ni wapi fedha za wasanii hao alikozipeleka kwa sababu kitendo cha kudhulumu
fedha hizo baadhi ya wananchi wanafikiri kimefanywa na chama cha mapinduzi CCM
wakati mzigo wote ulikabidhiwa kwa Steve Nyerere.
Steve alikua na la kujibu kuhusiana na tuhuma hizo na
kudai kuwa wote ambao hawakulipwa fedha taslimu ni wale ambao walikuwa hawana
mkataba ni wabeba mizigo .
‘’Alikwambia ana mkataba, huyo alikuwa hakuajiriwa na
alikuwa mbeba mizigo na wabeba mizigo wote wameshalipwa hakuna anayedai ‘’.
Hivyo Nyerere aliwaomba wananchi kupuuzia tuhuma hizo
kwani hazina ukweli ndani yake.
No comments:
Post a Comment