Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja
wa Kaitaba kujiweka kisawasawa na kuusoma uwanja huo ili kujiimarisha vyema
kabla ya kukutana uso kwa uso leo na Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa
miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja
wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Timu hii itacheza michezo miwili
ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa
Kagera. Mchezo wa kwanza utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na
kurudiana Aprili mosi, mwaka huu. Hata hivyo Mvua iliweza kunyesha na kukatisha
zoezi lao asubuhi na hatimae kurudi kwenye makazi waliyofikia jana baada ya
kuchelewa kufika Bukoba na kutoweza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.
Nayo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17
maarufu kwa jina la Serengeti Boys jana Jamatano walifanya mazoezi asubuhi saa
nne kujiweka tayari na mchezo wao wa leo na Timu hii ya Burundi.
Vijana wa Burundi wakiwa
wanateta jambo na kufurahia Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii ambako wanataraji
kupambana na Serengeti Boys leo hii kwenye mchezo wa kwanza wa Kirafiki wa
Kimataifa. Pia watarudiana siku ya Jumamosi.
Timu hii itacheza michezo
miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani
hapa Kagera. Mchezo wa kwanza utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na
kurudiana Aprili mosi.
Viongozi wa Timu hiyo yaBurundi wakiwaangalia kwa Makini Vijana wao ambako mapaka tunatoka kwenye Uwanja huo tuliweza kupata habari kuwa hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ameumia au ana jeraha la kuweza kumfanye awe nje ya Uwanja, Wote wako fiti kwa Mchezo wa leo dhidi ya Serengeti Boys.
Mvua kubwa ilinyesha na
kukatisha Tizi lao kwenye Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii na kwenda jukwaa
kuu.
Wakisikilizia Mvua...
No comments:
Post a Comment