Ally Kleist
Sykes (10 Oktoba 1926 Gerezani, Dar es Salaam - 19 Mei 2013 Nairobi, Kenya)
alikuwa mzalendo muasisi wa TANU na moja kati ya wapigania uhuru wakubwa wa
Tanganyika katika miaka ya 1950. Ally Sykes ndiye aliyemwandikia na Kumkabidhi
Mwalimu Julius Nyerere kadi ya TANU Na. 1.
Historia ina
kawaida ya kujirudia. Ally Sykes mmoja wa waasisi wa TANU, mmoja wa wale watu
wasiozidi takriban saba walikuwa katika kamati ya ndani ya TAA iliyounda TANU,
mmoja wa wafadhili wakuu wa TANU, mmoja wa askari kwa maana yake halisi kwa
kuwa ni Ally Syke ndiye TAA hadi TANU ikimtegemea kwa kutekeleza mambo ya
hatari dhidi ya Waingereza.
Ally Sykes
ndiye alikuwa akipewa kazi za hatari za kumwaga ‘’sumu na upupu’’ dhidi ya
serikali. Sumu na upupu huu yalikuwa makaratasi aliyokuwa akichapa nyumbani
kwake usiku makaratasi ambayo Waingereza waliyaita makaratasi ya ‘’uchochezi.’’
Waingereza na makachero wake walikuwa wanamjua Ally Sykes vizuri. Waingereza
walikuwa wakijua kuwa alikuwa na medali ya mlenga shabaha bingwa aliyopata Vita
Kuu ya Pili ya Dunia.
Huyu ndiye
Ally Sykes mzalendo muasisi wa TANU ambaye sahihi yake ndiyo iko katika kadi ya
TANU ya Baba wa Taifa. Harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na usaibu na
Nyerere
Inajulikana na wengi Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Julius Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952. Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes kwa utambulisho na hii ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao.
Inajulikana na wengi Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Julius Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952. Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes kwa utambulisho na hii ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao.
Mama yake
Nyerere Bi Mugaya hakuwa akipungua nyumbani kwa Mama Abdu Bi Mrurguru biti
Mussa Mtaa wa Kirk. Halikadhalika Maria Nyerere hakuwa akipungua nyumbani kwa aidha
kwa Bi Zainab mkewe Ally Sykes Mtaa wa Kipata au kwa Bi Mwamvua mkewe Abdulwahid
Sykes Mtaa wa Aggrey.
Wakati huu
Abdulwahid ndiye akiwa rais wa TAA na harakati za kuanzisha TANU zimepamba moto
achilia mbali hila na fitna za Waingereza kuwatokomeza viongozi shupavu wa TAA
kama Hamza Mwapachu, Dk. Vedast Kyaruzi, Dk.Wilbard Mwanjisi nje ya Dar es
Salaam kukivunja nguvu chama. Ndiyo maana TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954
Ally Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba 2, Nyerere namba 1, Abdulwahid Sykes
kadi yake namba 3, Dossa Aziz kadi namba 4, John Rupia kadi yake namba 7.
Kipindi hiki
Ally Sykes alikuwa Katibu wa Tanganyika African Government Servants Association
(TAGSA) na vilevile alikuwa mwakilishi wa chama hicho katika Kamati ya Uajiri
ya Serikali (Government Establishment Committee). Thomas Marealle ndiye alikuwa
rais wa TAGSA na Rashid Kawawa alikuwa mwanakamati. Wanasiasa hawa vijana Ally
Sykes akiwa mmoja wao wenyewe walijipa jina, ‘’Wednesday Tea Club’’ wakikutana
kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kutumia wakati ule kupanga mikakati
ya kuwang’oa Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Kupitia Ally, Abdulwahid na
Dossa Aziz Nyerere akaweza kujuana na wenyeji wa Dar es Salaam maarufu katika
hao ni Sheikh Hassan bin Amir, Mshume Kiyate, [[[Jumbe Tambaza]], Sheikh
Suleiman Takadir, Clement Mtamila, Bi. Titi Mohamed, Tatu biti Mzee na wengineo.
No comments:
Post a Comment