AJBAN
440A ni aina ya gari la Kivita maalum kabisa lililobuniwa na kutengenezwa na
kampuni ya magari ya Kivita iitwayo NIMR Automotives, iliyopo huko UAE (muungano
wa falme za kiarabu).
Gari
hili lina uwezo wa kubeba askari wanne, dereva akiwamo. Limetengenezwa kwa
teknolojia ambayo inalifanya haliwezi kupenyezwa na risasi hata ktk vioo vyake.
Pia lina teknolojia ya kisasa kabisa inayoweza kutambua Bomu lililotegwa
ardhini mita 100 kutoka linapoelekea au pembeni yake. Hivyo kumfanya dereva kukwepa kukanyaga Bomu hilo.
Hapo juu katika paa lake utaona
mtutu wa Heavy Machine Gun(HMG) ambapo 12.7mm rounds huweza tumika, mtutu huo
unatumia remote control. Pia linajilinda lenyewe kwa kuwa na uwezo wa kufyatua
"smoke grenades" 8 kwa mpigo au guruneti maalum zinazotoa moshi mzito
sana unaoziba eneo kubwa kwa haraka sana, na hivyo kumfanya dereva awakwepe
washambuliaji wake kwa kuhama eneo alilokuwepo kwa haraka.
Majaribio yake yamekuwa
yakifanyika huko Afghanistan, Iraq na mpakani mwa Pakistan na India, eneo la Kashmir.
No comments:
Post a Comment