Benki ya CRDB
imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kufungua akaunti ya
Malkia ambayo itakuwa ni yenye malengo yakinifu na manufaa kwa maendeleo kwa
wanawake.
Akizungumza
na Globu hii, Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya
CRDB Mary Gekura amesema kuwa akaunti hii ya Malkia inakuwa na malengo makuu ya
kumuwezesha mwanamke ili aweze kuwa na malengo yakinifu ya kujiendeleza
kiuchumi.
Mary amesema
kuwa, kampeni hii imeanza machi mosi na itakuwa ni endelevu na taratibu zake za
kufungua ni kwa kima cha chini cha shilingi cha elfu hamsini (50,000) na mteja
atatakiwa kuweka hela kwa muda wa mwaka mmoja bila kuzitoa.
Amefafanua
kuwa, ndani ya mwaka mmoja mteja anaweza kupata faida ya kutosha na kuanzisha
miradi mbalimbali.
Mkurugenzi wa tawi la
CRDB Water Front Donath Shirima (kulia) akiwa pamoja katika picha na
wafanyakazi wa tawi hilo kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani
Machi 08 mwaka huu.
Wafanyakazi wa wa tawi la
CRDB Water Front katika picha za pamoja kuelekea maadhimisho ya wiki ya
wanawake duniani Machi 08 mwaka huu.
Muhamasishaji wa kampeni
katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura akiwa anatoa maelezo
ya namna ya kufungua akaunti ya Malkia kwa wanawake inayolenga
kumnufaisha mwanamke.
Wateja wa benki ya CRDB
wakipata huduma katika moja ya madirisha ya benki hiyo tawi la Water
Front.Picha Zote na Zainab Nyamka
No comments:
Post a Comment