Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia, IFC imezindua kampeni ya Huduma ya kutumia fedha kwenda mtandao wowote bila gharama.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa kutoka Benki Kuu Tanzania, Bernard Dadi amesema huduma hiyo mpya itawanufaisha wananchi kupunguza gharama za kutumia fedha kwenda mitandao mingine.
Amesema kuwa kampeni hiyo itaongeza uelewa wa watumiaji simu za mkononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila gharama.
"Uwezekano huu wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mtumiaji, unatarajiwa kuongeza idadi ya watu wanaofaidika na huduma za kifedha nchini", amesema Dadi
Amesema kuwa kufanikiwa kwa Huduma hii ambayo kampeni yake ina lengo la kufikia watu milioni moja katika kipindi cha miezi sita kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya Kwanza duniani ambako makampuni ya simu yamekubaliana na wateja wao kutumiana fedha moja kwa moja.
Kampeni hiyo inayoongozwa na FEM Tanzania Ltd, inafanikishwa kwa msaada wa BOT, Taasisi ya Bill & Gates na Shirika la the Financial Sector Deepening.
Amesema, uchunguzi iliofanywa na IFC imebaini ukosefu wa uelewa wa Huduma hiyo miongoni mwa watumiaji kwa kukosa kuaminiana miongoni mwa makampuni ya simu na ushindani kwenye masoko.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, BOT, Bernard Dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari,hawapo pichani juu ya Huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote bila garama.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo y Taifa, BOT Bernard Dadi wa nne kutoka kushoto na wadau mbali mbali wa kampuni za simu nchini, wakiangalia onyesho la uzinduzi kutoka kwa Vijana wanaofanya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Huduma ya kutuma fedha kwenda mitandao yote.
Mkurugenzi Bernard Dadi wa pili kulia, Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedun na wadau wengine mbali mbali kutoka katika makampuni ya simu wakifuatilia kampeni za uzinduzi wa Huduma za fedha kwa njia ya simu bila garama yoyote.
No comments:
Post a Comment