Baadhi ya wasanii walioshiriki katika kampeni 2015 (Mama ongea na mwanao) wamepinga uvumi ulioenea kuwa wasanii hao waliofanya kampeni nchi nzima na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani hawakulipwa.
Akizungumza leo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, msemaji wa Mama Ongea na Mwanao, Ndumbago Misayo (Thea) amesema taarifa hizo za kutokulipwa katika kampeni sio za kweli na kinachofanyika ni kumchafua Makamu wa Rais, Mama Samia pamoja na kikundi cha wasanii walioshiriki kampeni za uchaguzi 2015.
Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yussuf (Baturi) amesema shutuma hizi zinatokana na baadhi ya wasanii kushawishiwa kuongea uongo kwa masilahi yao.
"Wasanii wote tumelipwa na mikataba ipo na haiwezekani mtu mwenye jina ukajitokeza mbele ya vyombo vya habari kuzungumza uongo wakati wewe ndio uliokuwa unalipa wenzio hicho kitu hakiwezekani" amesema.
Aliongeza kuwa kundi la Ongea na Mwanao bado lipo na linaendelea vizuri chini ya Makamu wa Rais , Mama Samia Hassan Suluhu.
"Msanii aliotangaza kuwa sisi wasanii hatujalipwa ni Wema Sepetu wakati yeye ndio alikuwa mlipaji wa kundi hilo.
Msemaji wa Mama Ongea na Mwanao, Ndumbago Misayo (Thea) akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa katika mitandao ya kijamii inayodai kuwa wasaanii waliozunguka na Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu hawakulipwa leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Yobnesh Yussuf (Baturi).
Makamu Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Yobnesh Yussuf (Baturi) akizungumza katika mkutano na waandishi habari juu ya madai ya kutolipwa katika kampeni za mwaka 2015 leo jijni Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa Mama Ongea na Mwanao, Ndumbago Misayo (Thea)
Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment