Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na
Usalama leo imefanya ziara ya kukagua mradi wa Vitambulisho vya Taifa; ambapo
mbali na kupokea taarifa ya utekelezaji pia walitembelea na kukagua kituo kikuu
cha Kuhifadhi, kuchakata na kuzalisha Vitambulisho vya Taifa -Data Centre.
Akizungumza wakati wa kukaribisha Kamati hiyo;
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema mpaka
sasa NIDA imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa pamoja na
changamoto kubwa ya fedha iliyopo.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo;
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Adad Rajab (Mb) amepongeza jitihada kubwa
zinazofanywa na NIDA na kwamba Kamati imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri
inayofanywa na NIDA na kwamba Kamati yake itaendelea kuishauri Serikali
kuongeza bajeti ya fedha kwa NIDA ili kuwezesha kukamilisha zoezi la Usajili
Vitambulisho vya Taifa, kwani manufaa ya kuwa na mradi huu kwa Taifa ni makubwa
katika Nyanja zote.
Wakitoa maoni yao wajumbe wa Kamati hiyo
wameitaka Wizara kuiwezesha NIDA na kuharakisha matumizi ya Vitambulisho vya
Taifa kielektroniki kwani tayari idadi kubwa ya wananchi wameshatambuliwa na
taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo.
“Kutokana na manufaa makubwa ya mradi huu kwa
Taifa, Serikali ihakikishe inatumia kila mbinu kuhakikisha matumizi
yaliyokusudiwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akimpokea Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba(Mb) mara baada ya kuwasili katika
ofisi za NIDA makao makuu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba (MB) akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge Mh. Adad Rajab (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo katika ofisi za NIDA
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakiongozwa na
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Adad Rajab (Mb) wakiwasili katika makao makuu ya
ofisi za NIDA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew W. Massawe akitoa ufafanuzi
kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama
kuhusu ubora wa Kitambulisho.
Afisa uzalishaji Vitambulisho vya Taifa Bw. Jeremiah Kivelege akitoa
maelekezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama
hatua za uzalishaji Vitambulisho vya Taifa walipotembelea kituo kikuu cha
Uhifadhi na uchakataji wa Taarifa (Data centre)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mh. Mwigulu Nchemba pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Bunge wakisikiliza jambo wakati walipotembelea kituo cha uchakataji
taarifa cha NIDA (NIDA DATA CENTER). Katikati ni Mh. Adad Rajab(Mb) mwenyekiti
wa kamati na kulia ni Mh. Sophia H. Mwakagenda(Mb) Mjumbe wa kamati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew W. Massawe, akisoma ripoti ya
Utekelezaji Mradi wa Vitambulisho vya Taifa kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya
Bunge. Kushoto ni Mh Sophia H. Mwakagenda(Mb) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nchi Mh. Balozi Simba Yahya.
Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mh. Adad
Rajab (Mb), akiongea jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya NIDA baada ya
kupokea taarifa ya Utekelezaji toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw.
Andrew W. Massawe. Kulia ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Kanali Mstaafu
Ramadhani Issa Abdallah(Mb).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akiwakaribisha
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili
NIDA kutembelea na kukagua maendelea ya mradi wa Vitambulisho vya Taifa.
No comments:
Post a Comment